Na Mwandishi Wetu

KATIBU  wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkuu wa Idara ya Organaizesheni Issa Gavu  amekuwa Mgeni rasmi katika Mkutano wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 - 2025 katika Jimbo la Mufindi Kusini linaloongozwa na Mbunge wa Mufindi kusini ambae pia ni Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile.

Pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya CCM  Ndg.  Gavu ametembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo barabara ya Nyololo kwenda Mtwago yenye urefu wa Km 40.38 inayotekelezwa na wakala wa TANROADS  inayogarimu Tsh 497,288,350.00 iliyopo kata ya Nyololo.

Gavu ameendelea na ziara yake katika kata ya Mbalamaziwa katika wilaya ya Mufindi kusini na kukagua Kontena lenye vifaa mbalimbali Vya Hospitali ya rufaa wilaya ya Mufindi vyenye thamani ya Tsh Bilioni moja nukta Nane (Bil 1.8)

Aidha Gavu amekabidhi baiskeli kwa watu wenye mahitaji maalumu katika jimbo la Mufindi kusini, amegawa mitungi ya Gas kwa vikundi vya mamalishe, Mashine ya uzalishaji wa  vifaranga zenye thamani ya Sh.Milioni 10.

Pia  amekabidhi mashine ya kufyatulia matofali yenye thamani ya Sh.milioni 15,vyerehani 10 vya kushonea kwa vikundi vya wakinamama pamoja na Pikipiki kwa kila Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Mufindi Kusini.

Gavu amemaliza kwa hotuba yake ya kuhitimisha katika Mkutano  Mkuu wa Jimbo la Mufindi kusini uliofanyika katika viwanja vya Mbalamaziwa na kuwataka viongozi wote ambao ni wakuchaguliwa waige mfano mzuri kutoka kwa Mbunge wa Mufindi kusini  David Kihenzile.

Aidha wajumbe wa Mufindi Kusini wamemshukuru Rais samia Suluhu Hassan kwa kumteuwa Mbunge wao kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa katika jimbo la Mufindi Kusini.




















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...