Na mwandishi wetu - MichuziTv Dodoma.
SERIKALI imeahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Tawi la Dodoma katika kutatua changamoto mbalimbali kwa kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi wa kutosha kuhudumia Watanzania.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule katika Hotuba yake kwenye Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyofanyika mapema leo hii Jijini Dodoma.
Na kuongeza kuwa kuwepo kwa miundombinu Bora ili kuendelea kuwahudumia Wanafunzi waliojiunga katika chuo hicho.
"Serikali pia inaahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha katika kutatua changamoto mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kuwa chuo kinakuwa kwanza wafanyakazi wakutosha wenye ujuzi na weledi kutosha kuhudumia Watanzania pili kuwa na miundombinu ya kutosha kuendelea kuhudumia Wanafunzi waliojiunga katika chuo hicho na pia chuo kuendeleza majukumu yake kwa ufanisi".
Aidha Mh Senyamule amewataka wahitimu na Chuo kwa ujumla kujitathmini juu ya elimu iliyotolewa na waliyoipata kuona ni namna gani inatumika kuongeza tija Serikalini na hata katika soko la Dunia hasa katika Zama hizi za Utandawazi.
"Hata hivyo tunaposherehekea Mahafali haya ya 49 tuendelee kujitathmini kama chuo na kama wahitimu kuhusu hatma ya elimu iliyotolewa na tuliyopa kuona namna gani elimu hii itatumika kuongeza tija Serikalini na mahalo pengine kwenye jamii hata elimu hiyo ikatumika kuongeza thamani Duniani.".
Pia Mh Senyamule ametumia nafasi kutoa ushawishi kwa Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa kuwakaribisha kuja kuweka makao makuu Jijini Dodoma kwani Wana eneo kubwa la Hekari 369 zilizopo eneo la Nala.
"Ukiangalia IFM ni kubwa Sana na Ina muda mrefu Sana ukiangalia Dar er salaam ni makao makuu lakini mmebanwa yani mkitaka kujitanua labda mkaanzishe sehemu nyingine iliyombali".
"Mimi nianze kuleta ushawishi nawakaribisha mje muweke makao makuu ya Chuo hapa Dodoma,kama Nala mna eneo kubwa hivyo mtaweka vitu kwa nafasi na kuweka ubunifu wa Wanafunzi ikiwemo maeneo maalum ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi katika kuimarisha utiaji wa Elimu"
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho cha Usimamizi wa Fedha Prof Josephat Loto katika Hotuba ameainisha changamoto zinazozikabili chuo hicho ikiwemo ukosefo wa mabweni, uhababa wa watendakazi na gharama za kupuangisha na kuomba Serikali katika utatuzi wa hayo.
"Kwasasa changamoto zinazotukabili sisi kama chuo ni pamoja uhaba wa Watumisha lakini pia gharama kubwa kukodi maeneo ya kufundishia na ukosefu wa Mabweni ya kulala Wanafunzi".
Prof. Loto ameongeza kuwa chuo hicho kimefanya mashirikiano na vyuo vya Kimataifa 12 ili kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa.
"Pia Mgeni Rasmi Chuo chetu tunafanya Mashirikiano na Vyuo vya Kimataifa 12 Nchi mbalimbali ikiwemo Ulaya, Asia na Afrika ya Kusini ikiwa lengo ni kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa"
Naye Mwenyekiti wa Baraz la chuo Prof. Emmanuel Mjema ameiomba Serikali kusaidia katika eneo la ujenzi ili waweze kujenga majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo na makao makuu ya Chama na Serikali.
"Tunaomba msaada wa Serikali ili tujenge majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo cha IFM na makao makuu ya Chama na Serikali katika eneo letu kubwa lililopo eneo la Nala".
Haya ni Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyojumuisha wahitimu 121 wanawake wakiwa 60 na wanaume wakiwa 61, ambapo Astashahada wahitimu ni 55, Stashada wahitimu 23 na Shahada ya Uzamili ni wahitimu 43.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...