News
Njombe

Spika wa Bunge la Tanzania Dkt .Tulia Ackson ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema kutokana na mabadiriko ya tabia nchi yaliyosababisha changamoto kubwa mkoani Manyara na kupelekea vifo kwa watu 89,wameweza kuchukua maoni ya wakulima wadogo juu ya matumizi ya kilimo ikolojia ili kupunguza athari hizo.

Dkt.Tulia amebainisha hayo mkoani Njombe wakati akifungua mkutano mkuu wa 28 wa maadhimisho ya miaka 30 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) unaofanyika mkoani humo.

Spika Dkt.amesema mabadiriko ya tabia nchi yameleta changamoto kubwa mkoani Manyara lakini anatoa shukrani kubwa kwa wakulima wadogo kufikisha hoja hiyo kwa uzito ambao ameweza kuisikiliza.

"Mmeleta hoja hiyo kwa uzito kabisa na mimi nimeisikia na mkurugenzi MVIWATA ameirejea tena kwamba tunaamini madariko ya tabia Nchi yanayotokea athari zake zinaweza kupunguzwa ikiwa tutashirikiana kwenye kilimo ikolojia"amesema Dkt.Tulia

Steven Luvuga ni mkurugenzi wa MVIWATA Tanzania amesema wakulima nchini wanachangamoto mbalimbali ambapo anaamini serikali inaendelea kutatua changamoto hizo hatua kwa hatua.

"Bado wakulima wanachangamoto mbalimbali ambazo tunaamini hatua kwa hatua zinatatuliwa na kwa kuangalia historia ya taifa letu na hali halisi ya jamii yetu ilivyo tunaamini wakulima wadogo watabaki kuwa moyo wa uzalishaji kwa muda mrefu"amesema Luvuga

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa pongezi kwa MVIWATA ambao ndio sauti ya wakulima kwa kufanyia mkutano wao mkubwa uliokutanisha zaidi ya wakulima 1000 kwa kuwa umesababisha watu wa Njombe kuchangamana na kujifunza kwa wengine kwa kuwa pia mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyoshikilia uchumi huku pia wananchi wake wakiwa ni wakulima kwa asilimia kubwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...