Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Jumatano Disemba 13 2023, amefika na kukagua Mradi wa Jengo Jipya la Hoteli ya Golden Tulip, hapo jirani na Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Kiembesamaki Mkoa wa Mjini – Magharibi, Unguja.

Katika Ukaguzi huo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Watendaji na Viongozi mbali mbali akiwemo Mkurugenzi wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Bw. Seif Abdalla Juma; na Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo, Bw. Hassan Mohamed Raza Hassanali Dharamsy.

Baada ya Ziara hiyo, Mheshimiwa Othman amekitembelea na kufanya mazungumzo na Kikundi cha Ushirika wa Ufugaji wa Nyuki (ZABA) huko Kitogani, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha, katika Ziara yake hiyo, Mheshimiwa Othman ameongozana na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Ushirika, Sekta Binafsi, na Asasi za Kiraia, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Bw. Ayoub mohamed Mahmoud.

Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Disemba 13, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...