Na Said Mwishehe-Michuzi TV-Chato
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdulurhaman Kinana ameeleza sababu za msingi ambazo zinasababisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kusifiwa na sababu kubwa ni namna ambavyo ameendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na hakuna mradi hata mmoja ambao umesimama.
Kinana ameyasema hayo leo Desemba 12, 2023 mbele ya wananchi wilayani Chato mkoani Geita wakati Mbunge wa Jimbo la Chato Dk.Merdard Kalemani akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika kipindi cha miaka miwili na nusu.
"Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi nzuri na wakati mwingine nimeona zimeanza kauli wanasema mbona mnamsifu sana Rais lakini lazima tukubaliane wakato wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi kuongoza ni kuonesha njia.
" Ukiwa na kiongozi mzuri , msikivu, mwenye kushirikiana na wenzake wakapanga na mambo yakawa kwanini tusimsifu , lazima tumsifu maana ndio anayetuongoza .Huko nyuma Baba wa Taifa tulikuwa tunasema zidumu fikra za mwenyekiti lakini fikra hazikuwa za Mwenyekiti ni za Chama cha TANU na CCM...
"Kwasababu gani? Ndio kiongozi wetu anafanya kazi nzuri.Rais Samia kwa muda mfupi sana amefanya kazi kubwa sana, ukimwambia Mkuu wa Mkoa hapa asimame aeleze fedha zilizoletwa katika mkoa huu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita basi nina hakika fedha zinazotolewa kipindi cha Rais Samia inaweza kuwa mara 10, " amesema.
Amefafanua jana alikuwa Mkoa wa Kagera ambapo ameelezwa Rais Samia amepeleka fedha Sh.bilini 260 , lakini kuna wakati alienda Rukwa ambapo aliambiwa amepewa Sh.bilioni 256 na Geita wamepewa zaidi ya Sh.bilioni 300 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Nanyi ni mashahidi chini uongozi wake mapato ya nchi yameongezeka , chini ya uongozi wake miradi yote mikubwa iliyoanzishwa na Hayati Dk.John Magufuli hakuna uliosimama .
"Hapa Chato kuna mradi umesimama?Miradi yote inaendelea na mingine imekamilika .Kila kitu kinaendelea.Dk.Magufuli aliacha ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) aliacha Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na sasa shughuli zinaendelea .
"Taarifa zilizopo umeme kutoka katika bwawa lile mwezi wa kwanza megawati 250 zitaingia kwenye gridi ya Taifa.Hivyo changamoto ya umeme itaendelea kupungua kadri megawati za umeme kutoka Bwawa la Mwalim Nyerere zinapoingia kwenye gridi ya Taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...