Kukamilika kwa kiwanda cha kuzalisha sukari Mkulazi kilichopo wilayni Kilosa mkoani Morogoro, kumetajwa kuwa kutawezesha kutoa ajira za moja kwa moja na za muda mfupi kwa vijana zaidi ya 5000.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini mfuko wa hifadhi wa jamii (NSSF) Mwamini Juma Malemi alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 100 na tayari kimeanza kazi ya uzalishaji wa sukari.

Aidha alisema kuwa sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho itaanza kupatikana madukani hivi karibuni na pia kutakuwa na duka maalumu litakalouza sukari kwa bei elekezi ya kiwanda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Mkulazi Dkt. Heridelita Msita alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi na amewahakikishia watanzania upatikanaji wa sukari ya kutosha kutoka kwenye kiwanda hicho.

Hata hivyo alisema kuwa hadi sasa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiweka oda kwaajili ya kupata sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa na manufaaa makubwa kwa wananchi na vijana kwa kupata ajira na kujiongezea kipato chao.

Ziara hiyo imefanyika lengo likiwa ni kukagua na kujiridhisha namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo mashamba ya miwa pamoja na mabwawa kwaajili ya umwagiliaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...