Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein, akitoa hotuba katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

MKUU wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kunahaja ya kuendeleza maeneo ya ardhi ya Chuo ambayo yapo jijini Dar es Salaam kwa kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo na zenye mwelekeo wa baadae.

Hayo ameyasema leo Desemba 14, 2023, Wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam. Amesema kuwa wanaweza kujenga ukumbi wao unaokidhi zaja na mazingira ya kisasa kwa kutumia shughuli zao rasmi na kukodisha watu wengine ili kujiongezea kipato.

Dkt. Shein amesema Chuo hicho kikiwa na ukumbi mzuri wa aina yake itakuwa ni jambo la maana na fahari kwa chuo na jamii inayowazunguka.

Licha ya hayo ameoumba uongozi wa Chuo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya kusomea katika eneo la Kituo cha Tegeta Ndaki ya Dar es Salaam ambako wanafunzi ngazi ya Shahada ya Kwanza wanasoma pia kutokana na uwingi wao watakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo.

Dkt. Shein ameeleza kuwa kutokana na kuwa na ndaki tatu sasa wanakamilisha ndaki ya Tanga ambayo itakamilika muda mchache ujao ili kuendelea kutoa elimu kwa maendeleo ya watu kama. Kauli mbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe inavyosema.

Kwa Upande wa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwegoha amesema kuwa kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kilisajili jumla ya wanafunzi 1,699 Ndaki ya Dar es Salaam.

Baadhi ya hao, ndiyo watakaohitimu katika mahafali hayo katika mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam jumla ya wanachuo 554 wamehitimu katika ngazi mbalimbali za kitaaluma na kustahili kutunukiwa shahada zao.

Katika ya hao, wahitimu 428 wametunukiwa Shahada za Umahiri na wahitimu 126 wamenukiwa Shahada ya Awali.

Kwa mwaka wa masomo 2022/23, idadi ya wahitimu wa Wanawake ni 311 sawa na asilimia 55.30 na wanaume ni 243 sawa na asilimia 44.70.

“Ni jambo la kujivunia na furaha sana kuona uwiano mzuri kati ya wahitimu wanawake na wanaume. Sisi kama Chuo Kikuu Mzumbe tutaendelea kupanua fursa na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuhakikisha kuwa uwiano huu unadumishwa mwaka hadi mwaka.” Amesema Prof. Mwegoha

Pia amewapongezawaitimu wote kwa kuhitimu masomo yao na amewaomba wakatumikie jamii na taifa kwa ujumla wakatumie vizuri maarifa, elimu na stadi walizopata Chuo hapo

“Elimu na stadi mlizopata kutoka Chuo Kikuu Mzumbe viwe chachu ya kuleta maendeleo chanya katika jamii inayowazunguka, taifa na dunia kwa ujumla.

Pia amewaomba wakawe mabalozi wazuri wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwa waadilifu na wachapakazi bora.
Mwanafunzi Bora Shahada ya Awali, Jonas John Baraka akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati wa mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakishangilia mara baada ya kutunukiwa Shahada zao. katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwegoha akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe  Prof. Cyriacus Binamungu akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam( DVC ARC) Profesa. Eliza Mwakasangula akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Ambapo amesema kuwa Kiongozi anaposhindwa kutatua changamoto, Changamoto inakuwa kiongozi.
Mhitimu Jonas John Baraka akizungumza katika Mahafali ya 22 ya chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...