Katika jitihada endelevu za kuchochea malipo kwa kidijitali, wateja wa Lake Energies sasa wanaweza kulipia mafuta kwa kutumia huduma ya kulipa kwa simu ya M-Pesa kutoka Vodacom katika vituo vyake vya mafuta nchi nzima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi wa M-Pesa, Mkurugenzi wa Operesheni za M-Pesa wa Vodacom, Tito Mbise, alisisitiza kuwa hii ni sehemu ya mkakati wa M-Pesa kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali kuhakikisha usalama, urahisi, na uwazi katika shughuli za biashara.

"Kupitia ushirikiano huu, mbali na kurahisisha malipo, wateja watarudishiwa 10% ya malipo yao ya mafuta wanapofanya malipo kupitia M-Pesa siku za Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili kuanzia msimu huu wa msimu wa sikukuu mpaka mwezi wa Januari.

 Tunaelewa kwamba watu wengi wanasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kuwatembelea jamaa na wapendwa wao wakati huu, hivyo suluhisho hili la malipo ya kidijitali linakuja wakati muafaka kwa sababu watu hawatalazimika kuwa na wasiwasi wa kubeba pesa taslimu ambazo huhatarisha usalama wao," alielezea Bw. Mbise.

Mbali na kurudishiwa pesa papo hapo ya kiasi cha 10%, kulipa katika vituo vya Lake Energies kupitia M-Pesa pia itaendelea kuwaongeza wateja nafasi za kushinda zawadi mbalimbali kupitia kampeni inayoendelea ya 'Sambaza Shangwe, Gusa Maisha'. Baadhi ya zawadi ni pesa taslimu, pikipiki, luninga za kisasa, simu janja, na router za 5G.

Ikihudumia soko la Tanzania kwa miaka 15 sasa, M-Pesa ya Vodacom inajivunia mtandao mpana wa wafanyabiashara wapatao 275,000 nchini kote, wanaokubali suluhisho la kulipa kwa M-Pesa. Ikiwa imejikita katika kurahisisha maisha ya kila siku ya wateja wake, inaendelea kuwa na ubunifu, hivi karibuni ikizindua huduma ya mkopo wa mafuta 'CHOMOKA', inayowawezesha madereva kujaza mafuta hata wanapokuwa hawana salio la kutosha barabarani, katika vituo mbalimbali nchini kote. Kupitia ushirikiano huu, wateja wa M-Pesa wanaweza kunufaika na huduma hii ya mkopo wanaponunua mafuta katika vituo vyote vya Lake Energies.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Lake Energies Tanzania, Fredy Mchau, aliongeza kwamba,

"Dhamira yetu daima imekuwa kuhakikisha kwamba wateja wanaotembelea vituo vyetu wanapata chaguzi mbalimbali za malipo. Ushirikiano huu na kampuni inayojitolea kutoa suluhisho za malipo ya kidijitali ni hatua muhimu kuelekea kufikia lengo hili. Tunatarajia kunufaika na mtandao mpana wa M-Pesa nchi nzima, ambapo huduma zetu pia zinapatikana.

Lake Energies ina vituo 139 kote nchini, pamoja, tunachangia kusaidia juhudi za serikali za kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali kwa kuhamasisha Watanzania wengi kubadilika kwenye malipo ya kidijitali na kuacha kubeba pesa taslimu ambayo inaweka usalama wao hatarini. Tunahakikisha wateja wote wanaokuja vituoni kwetu kupata huduma sasa wanaweza kulipa kwa M-Pesa."

Lake Energies, inayojulikana awali kama Lakeoil, ni mtoa huduma mkubwa wa suluhisho za nishati binafsi katika Afrika Mashariki na Kati, na vituo zaidi ya 540 katika eneo hili, ilianzishwa mwaka 2016, na ni kampuni inayokua kwa kasi zaidi katika sekta ya uuzaji mafuta.

Kushirikiana na M-Pesa ni sehemu ya mkakati wetu wa kutoa huduma na chaguzi bora kwa wateja wetu, wakipigania uchumi usio na pesa taslimu.

"Napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha Lake Energies kwenye familia ya M-Pesa, huduma inayoaminiwa na zaidi ya wateja milioni 17. Uwepo wenu umepanua wigo wa huduma na suluhisho zinazopatikana kwenye jukwaa letu. Pamoja, tukienea nchi nzima, bila shaka itakuwa faraja kwa wateja wetu ambao walikuwa wanatarajia kufanya malipo kupitia simu za mkononi lakini hawakuweza," alihitimisha Mkurugenzi wa Operesheni za M-Pesa wa Vodacom.
Mkurugenzi wa Huduma za Rejaraja wa Lake Energies Tanzania, Fredy Mchau (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni za M-Pesa wa Vodacom, Tito Mbise (kushoto) kwa pamoja wakijaza gari mafuta mara baada ya kuzindua huduma ya LIPA KWA SIMU katika kituo cha mafuta Samora Avenue jijini Dar es Salaam leo. Kupitia ushirikiano huo madereva wataweza kulipia kwa simu na kurudishiwa 10% ya pesa yao pamoja na kuweza kukopa mafuta kupitia huduma ya ‘CHOMOKA’ wanapokuwa hawana salio la kutosha.  

Mmoja wa mteja akilipia mafuta kwa kutumia huduma ya LIPA KWA SIMU katika kituo cha mafuta Samora Avenue iliyozinduliwa kwa ushirikiano baina ya M-PESA na Lake Energies jijini Dar es Salaam leo. Kupitia ushirikiano huo madereva wataweza kulipia kwa simu na kurudishiwa 10% ya pesa yao pamoja na kuweza kukopa mafuta kupitia huduma ya ‘CHOMOKA’ wanapokuwa hawana salio la kutosha.
Mkurugenzi wa Operesheni za M-Pesa wa Vodacom, Tito Mbise (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Rejaraja wa Lake Energies Tanzania, Fredy Mchau (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Idara ya Malipo wa Vodacom M-Pesa, Killian Kamota (wa kwanza kushoto) na Maneja Masoko na Mawasiliano, Matina Nkurlu (wa kwanza kulia) wakizindua huduma ya LIPA KWA SIMU katika kituo cha mafuta Samora Avenue jijini Dar es Salaam leo. Kupitia ushirikiano huo madereva wataweza kulipia kwa simu na kurudishiwa 10% ya pesa yao pamoja na kuweza kukopa mafuta kupitia huduma ya ‘CHOMOKA’ wanapokuwa hawana salio la kutosha. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...