Na John Walter-Manyara


Juhudi za kuwaokoa watu waliokwama kwenye Matope zimeendelea Vijiji vya Katesh na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara  baada ya Mafuriko kuyakumba maeneo hayo na kusababisha vifo vya watu 47 na wengine 85 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga watu zaidi wanahofiwa kufukiwa na matope baada nyumba na makazi yao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo kutoka Mlima Hanang'.Eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na Katesh ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya ya Hanang'.

Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika kwa muda.
Wakazi wa Hanang' wamesema hawajawahi kushuhudia hali kama hiyo na kwamba kwao hilo ni janga kubwa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia tukio hilo na kuzitaka mamlaka zote zihamishie nguvu wilayani Hanang kutoa msaada wa haraka.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...