Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa vituo vya Afya na Zahanati zilizokuwa tayari kujengwa na kuwa na vifaa muhimu zifunguliwe na kutoa huduma kwa wananchi ili kumaliza changamoto na makando kando yaliyopo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo hii katika hafla ya kukabidhi magari kwaajili ya Shughuli za Usimamizi wa huduma za Afya iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Na kuongeza kuwa yapo maeneo vituo vimekamilika na Zahanati zimekamilika lakini hazijafunguliwa na kusema mfano alipokuwa Sengerema kituo kimekamilika zaidi ya asilimia 97 na fedha za zipo lakini hakijafunguliwa zaidi ya mwaka mzima na kusababisha usumbufu kwa wananchi kufuata huduma mbali.
"Nitoe Tamko na hii itakuwani Mara mwisho nisiyakute Wala kuyasikia malalamiko ya kukuta kituo kimekamilika lakini hakijafunguliwa mnasababisha wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya wakati vituo vimekamilika, Mkurugenzi anajua na Mkuu wa Wilaya anajua lakini wanashindwa kuchukua hatua mpaka aje Mkuu wa Mkoa atoe maelekezo".
"Yale yaliyotokea Sengerema kituo kimekamilika kwa asilimia 97 lakini kimekaa mwaka mzima, na maelekezo haya nimeyatoa kwa muda mrefu lakini bado kila nikipita maeneo mbalimbali nakuta changamoto ni zile zile za kituo hakijafunguliwa,hizo changamoto na makando kando ni lazima tuyamalize".
Aidha Waziri amewataka Watumishi kufanya Kazi kwa moyo Mmoja na mkunjufu wanapo wahudumia wananchi kwani wananchi ndio mabosi wao.
"Pia jamani wahudumieni wananchi kwa furaha wanapokuja kwenu kutaka huduma waonesheni tabasamu kwani wananchi ndio mabosi kwani hata ukiangalia katika katiba yetu wananchi wametajwa Mara nyingi".
Pia hakuacha kuwa kumbusha Waganga Wakuu wa Wilaya kutembea katika malengo ya magari hayo yaliyotolewa leo.
"Nawakumbusha Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha magari haya waliyoyapa Leo yanatumika katika malengo kusudiwa na si vinginenyo".
Awali akimakaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma una uhitaji wa magari 97 ya kubebea wagonjwa yani Ambulance ambapo hadi Disemba 2023 Mkoa una jumla ya magari 27.
"Kwa Mkoa wa Dodoma mahitaji ya magari ni 79 ya kubebea wagonjwa (ambulance)ambapo hadi kufikia Disemba 2023 Mkoa una jumla ya magari 27, Mkoa umepokea pia magari matatu ambayo yamekwisha sambazwa katika halmashauri za Chamwino,Mpwapwa na Hospital ya Taifa akili Milembe".
Aidha amezungumzia ongezeko la vituo kwa Mkoa wa Dodoma ambapo amesema mpaka Sasa kuna ongezeko la asilimia 21 ndani ya miaka miwili.
"Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha miaka miwili vituo vimeongezeka kutoka vituo 429 mwaka 2021 Hadi vituo 545 mwaka 2023 hili ni ongezeko la vituo 116 sawa asilimia 21".
Magari yaliyotolewa Leo ni matano ambayo yanakwenda katika halmashauri tano za Mkoa wa Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...