Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
Mwanamke
mmoja (35-40)pamoja na mtoto wa miezi sita wamefariki dunia iliyotokea
Daru Mzumbwi Kisarawe ,baada ya basi lenye namba za usajili T 275 DRZ
aina ya tata kutumbukia kwenye mto na kusababisha vifo hivyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Pwani,Pius Lutumo alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo, Disemba 18 alasiri eneo la Daru Mzumbwi baada ya basi hilo,
lililokuwa likitokea Kigogo freshi, kuelekea Mloka kupitia Kisarawe
kupinduka na kuingia kwenye mto wenye maji.
"Basi
lenye namba za usajili T 725 DRZ aina ya Tata likifanya safari zake
Kigogo Dar es salaam- Mloka Rufiji ikiendeshwa na Juma Mohammed (51)
mkazi wa Pugu Dar es salaam liliacha barabara na kutumbukia
mtoni,"alifafanua Lutumo.
Lutumo
alieleza kwamba ,waliofariki dunia ni wawili akiwemo mwanamke mwenye
umri unaokadiriwa miaka 35-40 na mtoto wa miezi sita.
Alitaja chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kumudu gari kenye mteremko wenye kona kali.
Vilevile,
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge amefika hospitali ya wilaya ya
Kisarawe kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi waliokuwa katika ajali
hiyo.
Akithibitisha
kupokea majeruhi na miili ya marehemu ,Mganga Mkuu wa hospitali ya
wilaya ya Kisarawe Dkt.Risasi Rajabu, alieleza kuwa baadhi ya majeruhi
waliopata majeraha madogo wamesha waruhusu na wengine wanaendelea
kuwapatia matibabu.
Alieleza, wengine saba wamewapatia rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa Muhimbili.
Mkuu
wa wilaya hiyo, Fatma Nyangasa aliishukuru serikali kwa ujenzi wa vituo
vya dharura ambavyo leo hii kimeweza kuokoa maisha ya watu .
Kwa
upande wake majeruhi ambae ni mama was kichanga kilichofariki
Mwanahamisi Juma alieleza hakumbuki kilichotokea zaidi ya kujikuta akiwa
kwenye maji mtoni.
"Nilikuwa na mwanangu wa miezi sita lakini sijui anaendeleaje na hali yake, hadi hapo nitakapojulishwa na daktari"alieleza Mwanahamisi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...