Mashindano ya Robo mwaka mchezo wa pool Table yanaendelea mkoani Dodoma yakishirikisha jumla ya timu kumi na sita na washiriki binafsi zaidi ya mia moja na sitini.

Mashindano hayo yamekuwa na msisimko mkubwa kutokana na ushiriki wa vilabu kutoka mikoa mbali mbali Tanzania bara na Visiwani.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Pool TAPA Wilfred Makamba amesema lengo la kuchezwa kwa mashindano haya katika mikoa mbalimbali ni kuhakikisha mwamko unaongezeka nchi nzima ili kuibua vipaji vipya katika Pool.

 

Vilabu vinavyoshiriki katika mashindano haya ni kutoka Iringa, Mbeya, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma, pamoja na Zanzibar.

 

Vilabu vilivyoshiriki ni Zanzibar, Shooters, Iringa Combine, Mbeya Combine, Morogoro Combine, TIP TOP, Vegas, na Snipers. 

 

Washiriki wengine ni Waturuki, Warriors, Masti, Skylight A, Skylight B, Kikuyu, na Legend.

 

Washindi watakaopatikana katika mashindano ya robo mwaka Dodoma watajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, vikombe, pamoja na medali.

 

Hii ni mara ya pili kwa mashindano hayo kufanyika, kwa mara ya kwanza yalifanyika visiwani Zanzibar, timu ya TIP TOP ikitwaa ubingwa huo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...