MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi mifiko 100 ya saruji ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kata ya Misughaa za kujenga mabweni ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Dkt Alli Mohamed shein.

Akikabidhi Saruji hiyo msaidizi wa Mbunge Abdul Mdamo amesema ametumwa na mbunge kupeleka saruji hiyo ili waendelee na maandalizi ya ujenzi wa mabweni na hivyo kusaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi kutembea mwendo mrefu na pia kupandisha ufaulu.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya shule Mwalimu Philemo Vitalis ameeleza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa mabweni hayo kutasaidia kumaliza changamoto ya utoro na kuwavutia wanafunzi kimasomo na hivyo kuondoa changamoto zilizikuwa zinajitokeza hawa kwa watoto wa kike.

Akishuhudia makabidhiano hayo Diwani wa Kata ya Misughaa Selemani Sintoo amemshukuru mbunge kwa moyo wake wa kujitolea kwa kuwa amekuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya Kata yake na jimbo zima la Singida Mashariki kwa ujumla.

"Madarasa yamejengwa,barabara na madaraja vimejengwa, mawasiliano ya simu yameimarishwa kwani kabla ya kuingia kwenye ubunge kuna Vijiji vilikuwa havina mawasiliano ya simu kabisa,hakika Mhe Mtaturu ni mkombozi wa jimbo letu tunampa maua yake,".amesema diwani huyo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...