Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndugu Paul Makonda leo tarehe 1 December 2023 amemtembelea na kumshukuru Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally kwa kumuombea na kuanae katika nyakati zote alizozi pitia makonda kuendelea kupata Baraka zaidi.

Mwenezi Makonda amefanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano na Viongozi wa Dini katika kufanya kazi kwani anatambua ndio sehemu kubwa inayochochea uwepo wa Amani katika Taifa kutokana na maombi yao.

Kwa upande wa Mufti Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally amempokea na kumfanyia dua maalum ndugu Paul Makonda na kumuahidi kuendeleza ushirikiano na nakuombea katika kuhakikisha anafanya kazi zake vyema kwa lengo la kumsaidia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , kwa manufaa ya Watanzania na Taifa kwa Ujumla.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...