Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), linashiriki Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania ( NECTA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Akizungumza katika maonesho hayo,leo tarehe 30 Novemba 2023, Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Adolf Rutayuga amesema, NECTA ni wadau wakubwa sana wa NACTVET kwani wanafunzi wengi wanaojiunga na vyuo vya kati ni wale waliomaliza masomo ya kidato cha nne yanayoratibiwa na NECTA.

Amebainisha kwamba kwa kutumia kanzidata ya NECTA inayosomana na ile ya NACTVET, inawezesha utambuzi wa wanafunzi wenye sifa stahiki kuwawezesha kujiunga na vyuo vya kati na hivyo ushiriki wa NACTVET umelenga kuunga mkono na kupongeza mafanikio makubwa ya NECTA katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Aidha, Dkt Rutayuga amesema, NACTVET imeshiriki maonesho hayo ili kukutana na wadau mbalimbali ili kutoa elimu juu ya majukumu yake na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayosimamiwa na kutekelezwa na Baraza.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau na wananchi wote kwa ujumla kutembelea banda la NACTVET wakati huu wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA , yaliyofunguliwa rasmi leo tarehe 30 Novemba, 2023 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ambapo yatadumu kwa siku nne hadi tarehe 3 Desemba 2023.

Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Adolf Rutayuga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NACTVET katika Maonesho na  Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA  yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Afisa Udahili  NACTVET Levina  Lunyungu,  akitoa akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la NACTVET  katika Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA  yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya Matukio ya katika Banda la NACTVET kwenye  Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...