Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile ametembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)na kupata maelezo ya kina kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) namna kinavyotambulika kitaifa na kimataifa.

Mh. Kihenzile alitembelea Banda hilo Disemba 8,2023 katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha kuanzia Disemba 5-8, 2023.

Mh. Kihenzile alikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari ambaye alimweleza Mhe. Naibu Waziri mikakati ya TCAA ya kukitangaza chuo cha CATC pamoja na namna CATC ilivyopewa ithibati na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) kutoa mafunzo ya usalama katika usafiri wa Anga na kisha kupata maelezo kutoka kwa Godlove Longole Mkuu wa mafunzo ya Uongozaji Ndege ambaye alimweleza namna CATC inavyombulika kitaifa na kimataifa.

CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari alipokuwa anaelezea kuhusu Mamlaka hiyo inavyokisimamia Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) wakati wa kufunga Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha ulioanza Disemba 5 hadi 8, 2023.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole alipokuwa anaelezea kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa kufunga Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha ulioanza Disemba 5 hadi 8, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...