Na Pamela Mollel,Arusha 

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) yaungana na waandishi wa habari jijini Arusha kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya

Akifungua kikao hicho msaidizi wa katibu tawala na utumishi wa rasilimali watu David Lyamongi ,jijini Arusha katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Arusha aliwaasa waandishi wa habari kutoa ushirikiano pamoja na kuelemisha jamii ,kutoa taarifa mbali mbali za wauzaji na watumia wa dawa za kulevya 

Kwa upande wake msimamizi wa elimu ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Mkoa wa Arusha Shabani Miraji alitoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya madhara pamoja mikakati waliyoiweka ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaifa , kikanda na kimataifa 

Aidha aliongeza kuwa dawa za kulevya ni hatari katika jamii kwani  zinamadhara ya kifya,kijamii,kiuchumi, na kimazingira ya  hivyo wote tunapaswa kuyatokomeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...