Mkurugenzi wa usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini - Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki (kulia), akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA Jamal Kassim Ally (kushoto) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo zilizondaliwa na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia). ni Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed. DAR ES SALAAM

Ofisi ya Msajili wa Hazina imeng'ara kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika tuzo za uandaaji wa taarifa za fedha kwa mwaka 2023 katika kundi la Idara Huru za Serikali (Independent Government Department).

Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika hafla iliyofanyika mwisho mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi, wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini - Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki akiambatana na Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed, kwa niaba ya Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Mauki amesema kuwa ushindi walioupata utaongeza chachu ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuimarisha utendaji kazi katika Taasisi yao.

Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kutoa tuzo kwa Mashirika na Taasisi za Serikali zilizofanya vizuri kutambua kazi wanazofanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...