Na John Walter-Hanang'


Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG) wilaya ya Hanang' limetoa msaada wa magunia 40 ya mahindi kwa ajili ya waathiriwa wa maporomoko ya udongo, mawe na miti yaliyotokea jumapili desemba 3,2023 na kuathiri kata nne wilayai humo.


Muangalizi wa makanisa ya PAG wilaya ya Hanang' Mchungaji Philipo Siasi amesema wamekabidhi chakula hicho kuiunga mkono serikali kufuatia majanga yaliyotokea.

Aidha Mchungaji Siasi amewasihi watu wengine wenye mapenzi mema kuendelea kujitolea huku wale wenye ndugu zao wakawatoe kwenye makambi wakaishi nao.
Akipokea misaada hiyo leo Desemba 13,2023 Katibu mkuu, ofisi ya waziri mkuu, sera,Bunge na uratibu Dkt Jim James Yonazi amesema Kitendo kilichofanywa na Kanisa hilo kinawatia moyo waathirika wa maafa hayo na serikali.

Mbunge wa Jimbo la Jimbo la Hanang' Mhandishi Samwel Hhayuma ameishukuru serikali na wadau wote wanaoendelea kutoa faraja kwa misaada mbalimbali wanayoitoa.


Mbali na hivyo Mchungaji Siasi ameongoza maombi maalum kwa ajili ya kuiombea nchi ya Tanzania, Mungu ailinde na kuiepusha na majanga.
Hadi sasa miili iliyopatikana kufuatia maporomoko ya tope, mawe na magogo imefika 89.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...