BODI za Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) zimekutana na kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Desemba 4, 2023 Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa mkutano huo unashabaha ya kuendeleza sekta Mafuta na Gesi asilia nchini.

"Leo hii tumekutana kujadili, kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu ili tuweze kudhibiti na kuendeleza sekta hii muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu, tunatumaini baada ya kikao hiki tutaainisha mikakati yetu na kuifanyia kazi ipasavyo." Amesisitiza Mhandisi Sangweni.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA Adam Makame amesema kuwa mkutano huo umenuia kuweka mazingira bora kwa pamoja na kutangaza vitalu vya Mafuta na Gesi asilia ili kuweza kupata wawekezaji wengi nakuwezesha kupata wawekezaji wengi katika sekta hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Alfan Alfan amesema kwamba ushirikiano wa PURA na ZPRA kutoka Zanzibar itasaidia kujenga mahusiano ya muda mrefu katika kuhakikisha wawekezaji wanapatikana Tanzania Bara na Visiwani .

"Ushirikiano huu utaleta manufaa makubwa kwenye bodi zetu hizi mbili( PURA na ZPRA ) tutaweza kutangaza vitalu vyetu nakupata wawekezaji wengi hivyo sekta ya Mafuta na Gesi asili itazidi kukua nakuleta maendeleo kwa Taifa letu" amesema Alfan

Mwenyekiti wa bodi taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Mirza amesema kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza ili kujadiliana kwa pamoja nakuweka mikakati ya pamoja ya kunufaika na rasilimali ya Mafuta na Gesi asilia.
Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Desemba 4, 2023 mara baada ya mkutano wa kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.
Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar, Ali Mirza akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Desemba 4, 2023 mara baada ya mkutano wa kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.
Mkurugenzi Mwendeshaji Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar ZPRA, Adam Makame akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Desemba 4, 2023 mara baada ya mkutano wa kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...