
Maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike Jijini Mwanza Desemba 16, 2023 ambapo Mhe. Rais aliridhia mwaliko wa CWT Novemba 14, 2023 kuwa Mgeni rasmi na baadae CWT waliomba kubadili tarehe ya maadhimisho ifanyika Desemba 13 badala ya tarehe aliyoridhia Mhe. Rais.
Prof. Ndalichacho amebainisha hayo Desemba 12, 2023 Jijini Dar es salaam ambapo amesema Mhe. Rais alielekeza wataarifiwe tarehe waliyoibadilii atakuwa na jukumu linguine licha CWT kuendelea na maandalizi na kubadilisha hadi Desemba 16, 2023.
Aidha, Mhe. Ndalichako amewahakikishia walimu nchini kuwa serikali ya awamu ya Sita inatambua na kuthamini mchango wao na itaendelea kushirikiana na Wafanyakazi wote wakiwemo walimu ambao wanafanya kazi kubwa ya kuwalea na kuwajengea ujuzi watoto kwa ajili ya kujenga Taifa na ustawi kwa watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...