Chuo cha Taifa cha Utalii leo kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Hospitali ya Taifa Muhimbili yaliyojikita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya huduma bora kwa wateja.

Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Florian Mtey amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili inapokea wagonjwa wengi ambao kwa hakika ni lazima wapokelewe kwa ukarimu na watoa huduma wote.

Amesema chuo hicho kina dhamana ya kutoa mafunzo mbalimbali yakiwemo ya huduma bora kwa wateja, wahudumu mahsusi wa mapokezi ambao wanahitajika katika maeneo ya Hospitali, mafunzo ya mapishi n.k

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema ni ukweli usiopingika kuwa hospitali za umma nchini zimeboreshwa kwa kuwa na vifaa tiba, majengo mazuri lakini suala la huduma kwa wateja bado lina changamoto.

Amesema utiaji saini makubaliano hayo utasaidia kuendelea kuboresha huduma, kutoa fursa kwa wanafunzi kutoka chuo hicho kuja kufanya mafunzo kwa njia ya vitendo na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu utalii tiba.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...