Mwenyekiti wa Taifa wa Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa jamii Sospeter Bulugu akizungumza kabla ya kukabidhi msaaada wa Tsh Mil. 4.5 kutoka kwa mashujaa wa smaujata.

Mkuu wa wilaya ya Hanang'Janeth Mayanja akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Smaujata Taifa Sospeter Bulugu na baadhi ya mashujaa.
Mkuu wa wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa msaada kutoka kwa Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa jamii kutoka kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo( Smaujata )

Mwenyekiti Smaujata Taifa Sospeter Bulugu akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Hanang'msaada ukuotolewa na mashujaa wa Smaujata.


Na Vero Ignatus Manyara


Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo pamoja na Uongozi wa Taifa wametoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya mil. 4 kwa waathiriwa wa maafa wilayani Hanang' mkoani Mayara


Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa Smaujata Taifa ndugu Sospeter Bulugu kwa mkuu wa wilaya hiyo Janeth Mayanja, amemkabidhi jumla ya mifuko 25 ya saruji,mabati 20 misumari kilogram 10 pamoja ma mafurushi 24 ya nguo zilizotoka kwa mashujaa hao

Aidha Bulugu alisema wameweza kuwawapatia kama sadaka yao mbele za Mungu kwaajili ya kuwatia moyo na kuwafariji kwa sehemu wale wote waliofikwa na matatizo hayo pamojana kuondokewa na ndugu jamaa na marafiki katika maafa hayo.


''Tunatoa wito kwa Watanzania wote kuguswa na hali ya wenzetu kukosa makazi kila mmoja akitoa tutafanikisha kuwajengea makazi bora waathirika. "Kwa umuhimu huo tumekuja na ujumbe unaosema :''MASHUJAA tumeazimia kuijenga Hanang' ,tumekuja na hivi vifaa vya ujenzi kuthibitisha kauli yetu,Watanzania wote ni Mashujaa tunaomba kuungwa Mkono"alisema


Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Manyara Janeth Mayanja amewapongeza mashujaa hao kwa kuonyesha moyo wa kiutu na kuunga jitihada mhe. Rais kwa ndugu jamaa waliofikwa na maafa hayo.


Aidha mhe.Janeth amesema kuwa eneo kubwa lililoathiriwa na maafa hayo ya maporomoko ya tope,mawe,magogo na maji kutoka mlima Hanang,mkoa wa manyara yaliotokea alfajiri desemba 03,2023 kata ya Gendabi katikati a mji wa kateshi,ambapo mvua ilinyesha usiku wa kuamkia jumapili na kusababisha mafuriko ya tope zito katika eneo hiloKwa upande wake mkuu wa Idara ya Uhitaji, Maafa na Makundi Maalum Smaujata Iluminata Sanga amewashukuru sana mashujaa hao kwa kujitoa kwa hali na mali kwaajili ya kwenda kuwaona wana Hanang' waliofikwa na changamoto hiyo kubwa.


"Halikuwa jambo rahisi ila tunamshukuru sana Mungu ametusaidia kufanikisha jambo hili, nawapongeza na kuwashukuru masujaa wote endeleeni na moyo huohuo:
Iluminata Sanga mkuu wa IDARA ya Uhitaji maafa na makundi Maalum smaujata


Kwa upande wake Katibu wa mkoa padre Dennis Ngowi kwakweli tumewiwa sana na janga hili lilikotokea huku hanang' na tukaweza kuambatana kwa pamoja tunamshukuru mkuu wa wilaya HANANG kwa kutopokea kwa moyo wa chati nalishukuru jopo lote kutoa Arusha kwa moyo wenu.


Awali akifafanua wenyekiti wa Taifa Sospeter alisema kuwa Smaujata inafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za serikali zinazohusika katika kutoa haki, ambazo ni ofisi za Ustawi wa Jamii, polisi pamoja na Takukuru, hasa upande wa rushwa ya ngono, pamoja na Kutambua na kutengeneza mtandao wa jamii wenye uwezo wa kupaza sauti kupinga, kupambana na kutokomeza ukatili dhidi ya Jinsia Zote Wanaume, wanawake, watoto na wazee


Hivi karibuni ripoti ya serikali siku saba zilizopita kupitia Mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo na masemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi inasema kuwa hakuna miili zaidi ya iliopatikana na hivyo idadi ya miili inabakia kuwa 89 watu wazima 50 wanaume 21 na wanawake 29,na watoto 39 wakiume 19 na wa kike 20


Alisema kuwa miili 87 ilishatambuliwa na familia zao na kuchukuliwa kwaajili ya mazishi lakini miili miwili ya watoto wa kike mwenye umri wa mwaka moja na mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 3 bado haijatambuliwa na serikali itatumia utaratibu wa vinasaba (DNA)


Aidha taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa idadi kubwa walikuwa 139 ambapo waligawanywa katika hospitali mbili,a rufaa mkoa mjini babati,hospitali ya wilaya a Tumaini,na kituo cha afya cha Gendabi,wataalam wa afya waliendelea kutoa huduma kati a hao 2 ndio walipoteza maisha wengine waliruhusiwa kurudi majumbani.


kufikia leo tumebakiwa na wagonjwa 14 kama ifuatavyo:hospitali ya rufaa ya mkoa ina wagonjwa 9,hospitali ya wilaa a hanang ina wagonjwa 2 na kituo cha Afa cha gendabi kina wagonjwa 3,ambapo kambi za waathirika wakati fulani zilikuwa na watu zaidi ya 500 lakini hadi sasa wamebakia watu 36 tu


''Mgawanyo ni kama ufuatavyo shule ya msingi Ganana waathirika 4,shule ya msingi Gendabi kuna waathirika 9 na shule ya sekondari ya kateshi wapo waathirika 23 serikali inaendelea kuwaunganisha na ndugu zao hadi sasa serikali imefanikiwa kuwaunganisha waathirika 460 ambao wanatoka kati kaya 133na serikali inahakikisha kila kaya inayoondoka inapewa chakula cha kutosha na mahitaji yake kwa siku 30 na vitu vingine muhimu ambavyo wanavihitaji kuanza maisha yao


Serikali kupitia wizara ya Afya inaendesha kampeni za huduma za afya kusimamia afya kwa umma ambapo wataalam wa afya wameshatembelea kaya 6319 na kuzipatia vidonge 129,675 zimegaiwa vya kutibia maji,ili yawe safi na salama kwa matumizi,Wizara kwa kuumia wataalam wa afya ya akili wakiwa na mafisa ustawi wa ujamii,jinsia wanawake na makundi maalum jumla ya waathirika 2,144 walipatiwa huduma pamoja na ile ya kisaikolojia.


Aidha misaada ya fedha amesema wakati Rais akiwa ziarani kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi Dubai alipatuiwa kiasi cha fedha dola milioni moja na wahisani mbalimbali sawa na bilion 2.5 a Tanzania mbali na hizo mashirika ya umma na taasisi za umma kupitia kwa msajili wa hazina zilichanga shilingi billion 2.1 na nbali a hivyokulikuwa na mfuko wamaafa unaosimamiwa naofisi a waziri mkuu umefikisha shilingi milioni miamoja arobaini na tisa nalaki saba hamsini na saba elfu na mia tano,hii inafanya jumla ya fedha serikali iliyokusanya kufikia kiasi cha billion nne millioni mia saba arobaini na tisa laki saba hamsini na saba na mia tano


Vitu vilivakusanywa vilikuwa vina tahamani ya soko shilingi bilioni mbili milioni miamoja themanini na mbili laki sita na sitini mia nanae arobaini na nane ,aidha kamati ya kitaifa imekabidhi majukumu yake kwa mkoa wa manyara,baada ya majukumu hayo kukabidhiwa hata hivyo yote yataendelea kutekelezwa na wataalam watumishi wa wilaya mkoa pamoja na wale waliotoka kwenye serikalikuu katika wizara ykadhaa amabazo zina majukumu yake na yote itakuwa chini ya uratibu wa kamati ya maafa ya Taifa akisimamiwa na ofisi ya waziri mkuu.


MwishoMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...