Serikali imetangaza kuyafuta Mashirika manne ya Umma likiwemo Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) ambayo ilikuwa chini ya Wizara ya Afya.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo leo December 15,2023 akieleza hatua ilizochukua Serikali mara baada ya kuunganisha Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na kufuta baadhi ya Mashirika na Taasisi.

Prof. Kitila amesema pia Shirika la Elimu Kibaha linavunjwa na kuunda na Shule ya Sekondari Kibaha ama kwa jina ambalo Mamlaka husika zitaamua na Chuo Cha Ufundi “Kwa uamuzi huu Hospitali ya Tumbi Kibaha haitakuwa tena sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha bali Hospitali ya Mkoa wa Pwani na tayari Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya.

Amesema kuwa uamuzi huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kupitia hotuba yake ya Bungeni ya April 22 2022 ya kufanya mapitio na uchambuzi wa kina kwenye undeshaji wa Mashirika ya Umma, ili kuyafanya yaweze kujiendesha kwa faida.

“Hakuna Mtumishi atakayepoteza ajira yake, maslahi yote ya Watumishi ya umma katika Mashirika na Taasisi husika yatalindwa na kuzingatiwa kikamilifu kwa kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma, izingatiwe kuwa katika Mashirika na Taasisi nyingi za umma na Serikali kwa ujumla kuna upungufu mkubwa wa Watumishi wa umma,  hivyo, Watumishi wote ambao Mashirika na Taasisi zao zinaguswa na zoezi hili watapangiwa kazi nyingine katika utumishi wa umma na maslahi yao yatazingatiwa ipasavyo” amesema Prof. Kitila Mkumbo


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...