Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Kodi za Ndani - Walipakodi Wadogo, Edmund Kawamala (kushoto) akitoa tuzo kwa Mkurugenzi Mkuu wa SGA Guards (T) Ltd Eric Sambu baada ya kampuni kuibuka mshindi bora katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta Siku ya Tuzo za Kuwathamini Walipakodi Dar es Salaam.

SGA Guards (T) Ltd, kampuni ya ulinzi binafsi imepokea tuzo maalumu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuibuka mshindi katika Mkoa wa Kikodi Tegeta, kwa kuwa mlipaji kodi bora na kulipa kiasi kikubwa cha kodi kuliko kampuni zote binafsi kwa mwaka mzima.

Tuzo hiyo ilitolewa Siku ya Kumthamini Mlipakodi mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

SGA Guards (T) Ltd ilishika nafasi ya tatu kwa ulipaji kodi kwa mwaka 2022 na kwa mwaka huu ilishika nafasi ya kwanza.

Tukio hili lilihudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko, ambaye aliisihi TRA kuwaona wafanyabiashara kama wabia. SGA ilipongezwa kwa kuonyesha kwamba inawezekana kufanya biashara na kufuata sheria za kodi.

Akizungumza waakati utoaji tuzo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo alisema vigezo vigumu vilitumika kuwapata washindi wa kila kundi.

Miongoni mwa sifa zilizoangaliwa ni pamoja na kutangaza ulipaji sahihi wa kodi, ulipaji wa kodi zote kwa wakati, ulipaji wa kodi kwa kiwango kikubwa, ushirikiano na maofisa wa TRA na maoni ya kitengo cha uchunguzi wa mambo ya kodi.

Wakati wa kupokea tuzo CPA Eric Sambu, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa SGA, alipongeza juhudi zinazofanywa na TRA za kuwatambua walipakodi.

Alisema SGA ilikuwa kampuni binafsi ya kwanza kuanza kazi zake nchini mwaka 1984 na imeendelea kufanya vizuri katika maeneo yote kwa miongo minne baadaye.

“Tunalinda mambo yampasayo raia bora kwa njia ya kufanya kazi zetu ziendane na Mazingira, Jamii na Utawala (ESG) na utambuzi huu ni mfano kwa biashara nyingine Tanzania, kwa kuwa na utamaduni wa kutimiza wajibu kwa masuala ya fedha na uwazi,” alisema.

Mdhibiti wa Fedha wa SGA, CPA Jonathan Geleta, alisema kwamba tuzo waliyopokea ilikuwa ishara ya SGA kuweka kumbukumbu sahihi na kulipa kodi kwa wakati, akisisitiza matokeo chanya kwa mfumo wa taifa wa ulipaji kodi.

“Tunaona fahari kwa kuwa wazi na kulipa kodi, ambayo sasa imetambuliwa katika Mkoa wa Kikodi na TRA,” aliongeza.

SGA ni sehemu ya Kampuni Mama ya SGA ambayo imekuwa ikifanya kazi Tanzania kwa miaka 40 na sasa inafanya kazi nchi nzima katika kutoa huduma za ulinzi. SGA kwa sasa imewaajili Watanzania wapatao 5,000 kwenye mtandao wake katika idara mbalimbali. Pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana, SGA hushiriki katika shughuli mbalimbali za majukumu ya kampuni kwa jamii (CSR) nchini. Inashirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania kulinda sheria na amani nchini.

SGA ina vyeti vingi vya ISO, ikiwa ni pamoja na ISO 18788:2015, ambacho hutolewa kwa walipaji kodi bora na wanaofuata sheria na kanuni za nchi. SGA pia ni mwanachama wa Kanuni za Maadili za Kimataifa kwa Watoaji Huduma za Ulinzi Binafsi (ICoCA). Makao yake makuu ni Switzerland, na hulenga haki za binadamu na kufuata sheria zote. “Tunaamini kuendeleza viwango hivi ambavyo hutusaidia kuendelea. Tunayasihi makampuni mengine kwamba unafanya tu vizuri kwa kuonekana ukifanya vizuri,” alisema CPA Sambu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...