Shule ya Awali na Msingi ya Brookside iliyoko Kimara Suka ,Wilaya ya Ubungo , Mkoa wa Dare es Salaam imeshika nafasi ya kumi ki- Mkoa na  kuahidi kufanya makubwa zaidi.

Meneja wa Rasirimali watu na Utawala wa Shule hiyo Masanja Maduhu anasema kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha kwamba ndani ya miaka michache ijayo shule yao  inakuwa kinara miongoni mwa shule za Mkoa wa Dar es Salaam.

“Tumejipanga na nina wahakikishia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwamba tutaendelea kifanya vizuri na wazazi waendelee kutuamini na kuleta watoto wao kwenye shule yetu” Anasema Katika matokeo ya mwaka huu ya Darasa la Saba kwa mwaka 2023 Brookside imeshika nafasi ya kwanza katika Kata ya Saranga, nafasi ya pili katika Manispaa ya Ubungo na nafasi ya 10 Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya wazazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameipongeza shule hiyo kwa kutoa elimu bora na hatimaye kufanya vizuri Kimkoa.

“Kwa kweli naipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri na kulisaidia taifa kutoa elimu bora, anasema Magesa Bwire Mkazi  wa Kata ya Ukonga, Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Masanja anasema kuwa siri kubwa ya mafanikio ya shule yao ni ushirikiano baina ya wadau wote wa shule  Wazazi, Waalimu na uongozi bora.

Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shule ya Brookside , Masanja Maduhu  akizungumza katika moja ya hafla shuleni hapo .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...