Na Eleuteri Mangj, WANMM


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanya kikao na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi mikoa yote Tanzania Bara kutathmini siku 100 za uongozi wake tangu ameanza kuiongoza wizara hiyo.


Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 21, 2023 jijini Dodoma ambapo Mhe. Waziri Silaa amekutana Menejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kujitatnmini katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi bora ya ardhi.


"Hiki ni kikao kazi cha kutathmini siku 100 na kutengeneza mpango wa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi na kuwahudumia wananchi wetu" amesema Mhe. Waziri Silaa.


Waziri Silaa amewasisitiza Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuwa wana kazi ya kusimamia watumishi walio chini yao kwa kujipanga vizuri na wana uwezo kubadilisha jinsi sekta ya ardhi inavyoendeshwa nchini kote.


Waziri Silaa ameongeza kuwa Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wanachapa kazi vizuri katika mikoa yote, utendaji kazi wao utafanya taswira ya Wizara iende mbele kutekeleza maelekezo ya viongozi wa kifaifa na kuleta tija kwa watanzania.


Aidha, Waziri Silaa amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wataendelea kupokea na kuheshimu ushauri wanaoutoa kuhusu shughuli za sekta ya ardhi nchini.Awali akimkaribisha Mhe. Waziri kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa Menejimenti ya Wizara na taasisi zilizochini ya Wizara kwa kushirikiana na Makamishna Wasaidiza wa mikoa wapo tayari kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri kwa kuwa ndiye mwongoza njia ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.Mhe. Waziri Silaa ametimiza siku 100 katika nafasi hiyo ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 30, 2023 na kuapishwa Septemba 01, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...