NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wake dhidi ya Wydad Cassablanca kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi.

Simba Sc imefanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na mshambuliaji wao Willy Onana katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Wydad ilitawala mchezo huohasa kipindi cha kwanza licha ya kuruhusu mabao mawili ya haraka kufungwa ambapo waliweza kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini pongezi zimuendee kipa wa Simba Sc Ayoub ambaye aliweza kuokoa hatari nyingi langoni.

Simba sasa itakuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi lao akiwa amejikusanyia alama 5 huku wa juu yake ambaye anaongoza kundi ni Asec Mimosas akiwa na alama 7.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...