Na.Vero Ignatus,Arusha

Taasisi ya Nguvu za Atom Tanzania (TAEC) imeendelea kutoa mafunzo kwa watumiaji wa vyanzo vya mionzi katika nyanja ya Hospitali , vituo vya Afya,lengo likiwa ni uboreshaji wa utendaji kazi na usalama mahali pa kazi kwa watumiaji wa teknolojia ya mionzi

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Nguvu ya Atomu Tanzania (TAEC) Mkuu wa Idara ya Kiufundi ya kinga ya mionzi katika Esaya Sungita amesema kuwa Mafunzo hayo ni muhimu katika maeneo ambayo matumizi ya mionzi instumika na kuwataka kutilia mikazo yale yote watakayofundishwa kwani yatawasaidia katika utendaji kazi wao.

Esaya amesema Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuhakikisha usalama mahali pa kazi ikihusisha natumizi ya mionzi mahali pa kazi sambamba na kujilinda katika maeneo ya kiutendaji,kwani imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni Mamlaka ya udhibiti wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia,pia kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia hapa nchini

Amesema mafunzo hayo yanahusiana na jinsi ya kujikinga, namna ya kutumia teknolojia ya nyuklia katika huduma mbalimbali kwa hali ya usalama ili kuhakikisha kwamba wananchi wanalindwa ili wasiweze kupata madhara ya mionzi kwa kujua mbinu salama za kujikinga sambamba na kumkinga mgonjwa,pamojana wale wanaokuja kuwasaidia wagonjwa mahospitalini

''Kujikinga huko kunaanzia kwa mtoa huduma, kwa kujua mbinu salama za kujikinga sambamba na kumkinga mgonjwa anayemuhudumia pamoja na wale wanaokuja kuwasaidia wagonjwa pia waweze kuwa salama bila mionzi kutokanana kuwa katika maeneo hayo''alisema

Sungita alianisha kuwa mionzi hiyo inatumika katika sehemu mbalimbali haswa kwenye kutoa huduma za tiba , pamoja na uchunguzi wa magonjwa ikiwemo X-ray, kwaajili ya uchunguzi,ili mgonjwa aweze kupata matibabu kwa haraka zaidi, amesema sehemu nyingine ni ujenzi wa miundombinu ujenzi wa barabara,viwanda vya uzalishaji,uchimbaji wa madini,kilimo,ufugaji,uchimbaji wa maji,uchimbaji wa mafuta.

Amesema Kuwa baada ya mafunzo haya kwa wafanyakazi hao katika mahospitali pamoja na wale wa vituo vya Afya ,wanatarajia watakaporudi kwenye maeneo yao ya kazi wao wakawe jicho la kuangalia usalama kwenye maeneo yao yanaimarika

"Tunawatazamia ninyi kwenda kuwa washauri wa menejimenti kulingana na matumizi ya mionzi katika maeneo yenu, kwamba hatua gani zichukuliwe ili kuona usalama unaimarika" alisema

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo sister wa mashirika la upendo ya Mtakatifu Boromeo Singida ,katika hospital ya Sent Carola's mtingo Singida Marieta Lyakurwa amesema anategemea kunufaika na mafunzo hayo ambapo itamsaidia kwenda kutumia vyema elimu aliyoipata katika k kumlinda mgonjwa na kumsaidia apate huduma bora sambamba na kujilinda yeye mwenyewe kutokana na mionzi.

Nae Alfred Zelle kutoka hospitali ya wilaya ya Rombo amesema kuwa wamekuja kwenye mafunzo hayo lengo kuu likiwa ni kupata elimu juu ya usalama wa matumizi ya mionzi, ili wanaoorudi kufanya kazi zao wajue wanaenda kuwalimda vip wananchi sambamba na kutoa huduma iliyo nzuri na bora ili wanufaike pamoja na kuwalinda na kujilinda mwenyewe


Baadhi ya washiriki wa mafunzo juu ya usalama mahali pa kazi kwa watumiaji wa mionzi kutoka katika Hospitali pamoja na vituo vya Afya wakiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi ya Kandaya TAEC mkoa wa Arusha

Mkuu wa Idara ya Kiufundi ya kinga ya mionzi Esaya Sungita mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Nguvu za Atom Tanzania (TAEC) Prof.Busagala

Baadhi ya washiriki wa mafunzo juu ya usalama mahali pa kazi kwa watumiaji wa mionzi kutoka katika Hospitali pamoja na vituo vya Afya wakifuatilia mafunzo ya na maelekezo namna ya kutumia teknolojia ya mionzi katika ya Ofisi ya Kandaya TAEC mkoa wa Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...