Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi, amelitaka Shirika la umeme nchini (TANESCO) kujali na kuzingatia maslahi ya watumishi wake ili kuongeza ufanisi na ubunifu katika kutekeleza majukumu yao.
Katambi, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati
akifungua mkutano wa Baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili lenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Amesema ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa watumishi ndani ya shirika hilo maslahi ya watumishi yanapaswa kupewa kipaumbele ili kuongeza uwajibikaji.
“Ili kuongeza ufanisi wa shirika letu hili ambalo tunalitegemea katika uzalishaji wa umeme mnapaswa kuzingatia maslahi ya watumishi wenu kwa kuwapa motisha, posho, kupandishwa vyeo ili kuwaondolea stres watumishi na kuongeza tija an ubunifu katika shirika hili tunalolitegemea kwa kuzalisha nishati ya umeme nchini”amesema Katambi
Aidha, Katambi amewataka watumishi wa shirika hilo kuzingati wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu kabla ya kudai haki zao.
“Kabla ya kudai haki zetu lazima tuangalie wajibu wetu katika maeneo yetu tumeutimiza kwa ukamilifu suala la umeme nchini ni jambo la muhimu sana hivyo tunapaswa kutimiza majukumu yetu ili kuondoa malalamiko ya mgao wa umeme nchini”amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Gissima Nyamo-hanga amesema mkutano wa baraza hilo utafanyika kwa siku mbili ukiwa lengo la kujadilia mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya kiutendaji.
Pia amebainisha maagizo yote yalitolewa na Naibu Waziri Katambi watayafanyia kazi ili kuongeza ufasi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa watumishi wao.
“Baraza kuu la wafanyakazi ni chombo ambacho pia majukumu yake ni kuangalia maslahi na haki za wafanyakzi hivyo pia katika kikao chetu tutakwenda kujadili masuala ya maslahi kwa watumishi na haki zao”amesema
Hata hivyo, akizungumzia kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme nchini amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na zimeongeza uzalishaji katika vyanzo vilivyopo nchini ikiwemo Mtera,Kihanzi na Kidatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...