Na Said Mwishehe, Michuzi TV
NCHI za Tanzania na Malawi zimesaini mkataba wa ushirikiano kuhusu ushoroba wa kusafirishaji baina ya nchi hizo mbili huku ikielezwa Malawi itatumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo

Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaaam ambapo kwa upande wa Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na kwa upande wa Malawi amesaini Waziri wa Usarishaji.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo wa ushiriakino wa ushoroba wa usafirishaji, Waziri Profesa Mbarawa amesema nchi ya Malawi imekuwa mtumiaji wa bandari ya Dar es Salaam.

"Kwa kuwa mkataba huu ulikuwa wa muda mrefu tumeweza kusaini upya kwa lengo la kuhakikisha kwamba sasa unafanya vizuri zaidi.Serikali imejenga miundombinu mingi kwaajili ya kuboresha ushoroba huo wa usafirishaji kati ya nchi hizo mbili, " amesema.

Pia amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya maboresho makumbwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kuanzia gati namba moja hadi namba saba huku akifafanua kuwa wamejenga gati maalum kwaajili ya gati namba zero.

Amefafanua katika kuendelea kupanua uwezo wa bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha utoaji huduma ndio maana wameamua kutoa nafasi kwa sekta binafsi kufanya uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kusisitiza wanafanya hayo yote kuhakikisha wanaongeza ufanisi kwa ajili ya bandari hiyo.

Akizungumzia Bandari ya Mtwara Profesa Mbarawa amesema Serikali amefanya mabadiliko makubwa ikiwemo kujenga gati la kisasa mbali na urefu takribani mita 300 inafanya kazi na wameweka vifaa vya kisasa.

Pia amesema wiki inayokuja wanatarajia kusaini mkataba kwaajili ya ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ambayo ni muhumi kwa wakazi wa Ziwa Nyasa.

"Bandari hii ni muhimu kwaajili ya watu wa Malawi na jitihada zote zinafanywa kuhakikisha wanafungua ushoroba huo kati ya Tanzania na Malawi

Pamoja na mambo mengine imeelezwa kwa upande wa Malawi utarahisisha upatikanaji wa bidhaa kwa nchi yao wakitumia korido ya Mtwara ambayo itapunguza gharama ya usafirishaji bidhaa na hivyo wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu.

Akizungumzia faida ya mkataba huo, Profesa Mbarawa amesema mkataba huo unafaida kwa Tanzania na Malawi huku akieleza kwamba kwa mwaka 2022 mzigo ulihudumiwa na bandari ya Dar es Salaam kwa nchi ya Malawi ulikuwa takribani ya zaidi tani 500, 000

"Lakini ukilinganisha na mwaka 2018 kumekuwa na ongezeko kubwa hivyo tunataka ongezeko lifikie hadi tani million moja au mbili na hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam

" Tumekuwa tukisaini mikataba kwaajili ya kuifungua Bandari ya Dar es Salaam japo kuna ushindani na tukipanga vizuri kama tunavyoendelea na ujenzi wa miundombinu hakuna mtu ataweza kushindana. Kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi na Kazi za Umma nchini Malawi ametumia nafasi hiyo kuelezea manufaa ambayo yanakwenda kupatikana kwa nchi zote mbili baada ya kusaini mkataba huo unaotoa fursa kwa nchi yao kutumia bandari ya Dar es Salaam.

Aidha amesema anaamini mkataba huo waliousaini utasaidia kufanya kazi kwa pamoja kati ya Tanzania na Malawi na kurahisisha usafirishaji.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Tanzania Profesa Makame Mbarawa(kulia) na Waziri wa Uchukuzi na Kazi za Umma Jacob Hara(kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano kuhusu ushoroba wa usafirishaji katika Bandari ya Dar es Salaam.Wanaoshuhudia ni wanasheria wa nchi hizo mbili

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) na Waziri wa Uchukuzi na Kazi za Umma Jacob Hara( kushoto) wakiwa wameshika mkataba wa ushirikiano baada ya kuusaini jijini Dar es SalaamMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...