MWANDISHI WETU, SIMIYU

CHAMA cha Wachimbaji Wanawake Mkoa wa Simiyu, (TAWOMA) kimemuomba radhi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu Emmanuel Silanga ambae ni mshauri wa maridhiano pamoja na Muwekezaji wa Mgodi wa namba 10, Dutwa, Daudi Emmanuel, kwa madai ya kumchafua kutokana na kudanganywa na wanasiasa na kuandamana, kufanya fujo, huku wakitambua hawana leseni ya umiliki wa mgodi huo.

Hata hivyo, taarifa kutoka katika Ofisi za Madini Mkoa wa Simiyu zinaeleza kuwa Wachimbaji hao Wanawake hawana leseni ya kumiliki wa mgodi huo na kwamba hawakuwa na sifa za kuwepo katika kwa sababu hawakuomba leseni licha ya wao kulalamika kuwa wapo kihalali.

Muwekezaji huyo akizungumza na Waandishi wa Habari alisema hakuna mgogoro wowote uliyokuwepo kati ya wachimbaji hao na yeye, bali ni changamoto chache zilizotokea ambapo wachimbaji hao hawakukaa nae pamoja na kukubaliaana baadhi ya mambo na kuwaomba kwamba waache kutumiwa na wanasiasa wasioitakia mema nchi, kwani wao walitambua wazi kwamba hawakuwa na leseni ya eneo hilo la mgodi.

Alisisitiza kwamba kilichopo ni wachimbaji hao kutumiwa na wanasiasa wasiokitakia mema Chama cha Mapinduzi na kuwa chanzo cha Migogoro isiyokuwa na tija na kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo haina afya kwa maendeleo ya taifa.

Kufuatia hatua hiyo ya wachimbaji hao kumuomba radhi mwekezaji huyo, wachimbaji hao wameruhusiwa na mwekezaji huyo kusimamia na kuendelea na uchimbaji katika mgodi huo na kwamba yeye atakuwa akipokea taarifa za uendeshaji wa mgodi kutoka kwao na Meneja Wake.

“Naomba ifahamike kuwa hakuna mgogoro uliyokuwepo kati yangu na Wachimbaji hawa, Mimi nawapenda sana Wachimbaji Wanawake wa Mkoa wa Simiyu. Nimewapa ruhusa ya kusimamia mgodi, nitakuwa nikipokea taarifa za uendeshaji kutoka kwao,”alisema Emmanuel na kuongeza:

“Nawaomba sana Wachimbaji wasikubali kutumiwa na wanasiasa wasio kitakia mema chama.Kama kuna mambo ya msingi ni vema tukaketi pamoja tukazungumza ili kuondoa migogoro isiokuwa na tija na pia endapo mtashindwa kuelewana ama mkipigana tena kwa sababu ya usimamizi sina budi kuwaondoa katika usimamizi ili mbaki kuwa wachimbaji tu.”

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Emmanuel Silanga alisema kuwa kutatuliwa kwa mgogoro huo ni juhudi za kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu katika kuwawezesha akina mama ili waweze kujiinua kiuchumi kwa maendeleo ya taifa la leo na kesho.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia haipendi kuona akinamama wakiwa wanahangaika kwa sababu wao ndio uti wa mgongo wa familia ndio maana tunatamani kuona wakiwa vizuri kiuchumi kwa manufaa ya taifa la sasa na kesho kwa sababu wao ndio walezi wakuu wa familia, serikali inawajali ndio maana imeamua kusimamia hili ili kuhakikisha hakuna mgogoro tena”.Alisema Silanga

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Ismail Nawanda akizungumzia suala hilo, alisema wameketi pamoja kati ya muwekezaji huyo na wachimbaji hao wanawake na kwamba muwekezaji ambaye ndie mwenye leseni amekubali kuwaruhusu kusimamia mgodi huo.

“Tumeketi pamoja kati ya mwekezaji na wachimbaji Wanawake, tumemaliza changamoto zilizotokea na sasa wameruhusiwa kusimamia mgodi huo. Na kuanzia Jumatatu kazi za uchimbaji itanzaa rasmi mgodini,”alisema Dk Nawanda.

Mara baada ya kuruhusiwa kusimamia mgodi huyo na kuendelea na kazi zao za uchimbaji wa dhababu, Mwenyekiti wa Wachimbaji (TAWOMA), Mary Chacha amemshukuru Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Emmanuel Silanga kwa kuwasaidia kurejea katika majukumu yao ya usimamizi wa mgodi na kwamba wamempongeza kwa kuwajali wachimbaji wanawake wa Mkoa wa Simiyu.

“Kwa niaba ya wanawake wachimbaji napenda kumshukuru mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Silanga kwa kutusaidia katika kumaliza huu mgogoro kwa njia nzuri ya maridhiano ya pande zote mbili na sisi kurejea katika majukumu yetu tunamshukuru sana yeye pamoja na Mkuu wa Mkoa kutusaidia katika hili” alisema Chacha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...