*Ni katika uwasilishwaji wa hesabu zinazokidhi viwango vya NBAA

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yangara nafasi ya kwanza kwa katika uandaaji bora wa Hesabu mwaka 2022.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

TRA tangu imeanza kushiriki imekuwa ikishika nafasi mbalimbali katika Tuzo hizo za NBAA

TRA imeshika nafasi ya kwanza ya uwasilishwaji bora wa hesabu mwaka 2022 ikishindanishwa na mashirika mengine ya Umma ya Udhibiti wa kitumia viwango vya kimataifa vya kutayarisha hesabu

Mara baada ya yakupokea tuzo hiyo, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Alphayo Kidata amesema ushindi huo umewapa chachu ya kuendelea kuboresha utendaji wake katika maeneo wanayosimamia na utoaji wa huduma bora zinazokidhi viwango wa ndani na nje ya nchi.

“Ushindi huu unatoa ujumbe wananchi kuwa tunanachosimamia kipo salama na fedha zao hakuna zilizopotea na tutaongeza nguvu zaidi kuhakikisha tunakuwa kioo bora kwa wananchi.

Amesema shindi huu si wa mara ya kwanza kwa TRA kuibuka kidedea na kufanya kuendelea kujiweka imara zaidi.

Kidata amesema mafanikio hayo yameendelea kuchochea kuimarika kwa utendaji ndani ya taasisi hiyo.

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza wa jumla ya umahiri katika uaandaji wa taarifa za hesabu zinazozingatia ubora wa kimataifa (IPSAS) kwa mwaka unaoishia 2022 pamoja na tuzo ya mshindi wa kwanza kwa Mashirika ya Umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA Jamal Kassim Ally (kushoto) wakati wa hafla ambayo imeandaliwa na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...