NYOTA wa Muziki kutoka Nigeria, ambaye pia ni mtayarishaji, mpiga vyombo vya muziki Pheelz, leo ametoa EP ya ya Pheelz Good( Triibe Tape) yenye nyimbo 4 ambazo kwa sasa zinapatikana kupitia Warner Records.

EP inangoma kama JOY' aliyomshirikishwa gwiji wa Afrobeats Olamide, kwa mujibu wa Pheelz anasema ‘’Joy’ ni wimbo maalum kwangu kwa sababu mimi na Olamide tumekuza udugu wetu na tumekuwa marafiki kwa miaka mingi"

Pia EP hiyo ina ngoma nyingine kama 'JELO' ambayo ilitoka muda kidogo na amemshirikisha Young Jonn, na pia kuna remix of “JELO” akimshirikisha Lekyz na Henry X, na ngoma nyinginr ni “Riddim & Blues.”

Akizungumza leo Novemba 4, 2023 amesema "Triibe Tape ni kazi nzuri ya Kabila na baada ya hapa, nitasafiri kote ulimwenguni kuungana na mashabiki. Kwa hivyo, ni mradi wa sisi kushirikiana nao kwenye jukwaa., na kuburudika na mziki mzuri".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...