-Ni baada ya kushika namba tatu mkoa wa Dar

Shule ya Msingi Lusasaro iliyoko Tabata Kisukuru Jijini Dar es Salaam imedhamiria kuongoza matokeo ya darasa la saba kitaifa mwakani baada ya kushika nafasi ya tatu mkoa wa Dar es Salaam.

“Tunataka kuongoza kitaifa , uwezo huo tunao kama tumeshika namba tatu Ki-mkoa kwanini isiwe kitaifa? Anahoji Louis Lugata, Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo.Louis anasema kuwa ushirikiano baina ya mamlaka zinazosimamia Elimu, Waalimu wazazi na wanafunzi ndiyo siri ya mafanikio yao.

Katika matokeo yaliyotangazwa hivi Karibuni na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa Darasa la Saba mwaka 2023 shule hiyo ya Mchepuo wa Kiingereza imeshika nafasi ya tatu ki- mkoa na kuongoza kwenye Kata ya Tabata Kisukuru.

Anasema kuwa wamejiandaa kuzalisha kizazi bora cha wahitimu ambao watakuja kulisaidia taifa siku za baadaye kwa kuibua na kukuza  vipaji vya vijana na hatimaye kuja kuwa viongozi bora.

Naye Mwalimu wa Taaluma shuleni hapo Maganiko Simon anabainisha kuwa wamedhamiria kuzalisha vijana ambao watakuwa na uwezo wa kufikiri vizuri na wabunifu ambao wataifanya Tanzania kuwa nchi bora.

“Sisi tunataka kuifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa kuzalisha vijana ambao wana uwezo wa kufikiri na kuwa wabunifu” anasema.

Anabainisha kuwa taifa ili liendee linahitaji watu watu wenye ubunifu na hatimaye kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwa ubunifu wao.Shule ina panga kijikita katika kuibua vipaji kwa vijana na kwani Dunia ya sasa vipaji vinalipa sana na kuongeza pato la taifa, watawekeza zaidi katika masomo ya kumpyuta na miundombinu ya michezo mbalimbali anasema Mgata.

Louis Lugata, Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Msingi Lusasaro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...