Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Màendeleo (UNDP) limekabidhi gari moja aina ya Ford Ranger kwa Jeshi  la Magereza nchini kwa lengo la kuliwezesha kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa ufanisi.

Akikabidhi gari katika Ofisi za UNDP Dar es Salaam, Meneja utawala wa Shirika hilo Victor Kida amesema gari wanatambua majukumu ya jeshi hilo hivyo msaada wa gari hiyo utalilisaidia Jeshi hilo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

" Tunatambua mchango mkubwa wa Jeshi la Magereza katika utendaji wake ndani ya Taifa, tunaamini kwa msaada wa gari hili utasaidia kuongeza ufanisi kiutendaji" amesema Meneja huyo 

Aidha akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Mzee Ramadhani Nyamka, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Juma Mwaibako pamoja na kuishukuru UNDP kwa msaada huo amesema gari hilo litatumika kama inavyostahili na kuongeza kuwa wao kama Magerezaw anauheshimu msaada huo.

"Tunawashukuru ndungu zetu wa UNDP kwa msaada huu ambao kwetu una thamani kubwa, tunaahidi kulitunza gari hili ili liweze kudumu kwa muda mrefu ili liwe alama muhimu ya kumbukumbu kwetu, " amesema ACP Mwaibako

Aidha amesema wao kama taasisi muhimu ya Serikali wanawakaribisha wote wenye malengo ya kutoka misaada mbalimbali itayolisaidia Jeshi hilo kuzidi kuongeza ufanisi huku akisisitiza kuwa milango ipo wazi kwa wote wenye nia hiyo.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...