*Serikali yaahidi kushirikiana bega kwa bega


Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV

Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema viongozi wa kimila wana mchango mkubwa katika kutoa elimu kwa wananchi masuala mbalimbali na serikali inawategemea.

Msigwa ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Kimila iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema viongozi wa kimila waendelee kushirikiana na serikali katika kuwahamasisha Watanzania kutumia takwimu zilizotolewa baada ya Sensa ya Watu na Makazi inatoa mwelekeo kimaendeleo.

Katibu Mkuu Msigwa amesema matokeo ya Sensa ni muhimu kwani ndiyo dira inayoongoza kufanya maamuzi ya msingi na kujibu changamoto zinazowakabili wananchi ambao ndio viongozi wa kimila mnawahudumia

Amesema matokeo hayo yatawasaidia viongozi wa kimila kujua jamii waliyonayo na jinsi ya kukaa nayo katika kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo yao.


“Niwapongeze sana machifu na viongozi wa kimila kwa kuwa sehemu ya serikali kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo zinazotekelezwa na serikali na imani yangu inanituma mafunzo yanayotolewa ya matokeo ya sensa matapata ufahamu hali halisi na kufanya maamuzi katika kutoa ushauri katika maeneo yenu,”alisema.

Kamisama wa Sensa ya Watu na Makazi ,Anna Makinda amesema ni vizuri viongozi hao wakajua matokeo kwani wanataka Watanzania wote wazungumze lugha moja ya kupanga maendeleo

Amesema matokeo hayo ni ya kihistoria kwa sababu hakuna nchi iliyofanikiwa katika Sensa kama Tanzania kwa kuhesabu watu wengi haijawahi kutokeo

Kwa upande wake, Kiongozi wa Machifu nchini, Antonia Sangalali alisema machifu wapo tayari kushiriki kikamilifu kama walivyofanya kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi.

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akizungumza wakati wa akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi wa Kimila  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 

Kamisaa wa Sensa Spika Mstaafu Anne Makinda akitoa maelezo kuhusiana matokea ya Sensa katika  Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Kimila iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 

Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Antonio Sangalali akitoa maelezo kuhusiana machifu wanavyoshiriki shughuli za Serikali kwenye  Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Kimila iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu wa NBS Ruth Minja  akizungumza kuhusiana mafunzo hayo namna yanavyoratibiwa na NBS  kwenye   Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Kimila iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 

Sehemu ya Viongozi wa Kimila wakiimba wimbo uliotumika katika sensa ya Mwaka 2022 uliotungwa na Mwenyekiti wa umoja wa Machifu kwenye kwenye Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa Kimila iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...