Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO.

MKUU wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro amewahamasisha wananchi wa ndani na nje ya wilaya hiyo kutembelea na kujionea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Hifadhi ya Msitu wa Asili Magamba.

Ametoa wito huo katika uwanja wa Nyerere Square kwenye maonesho ya vivutio vya utalii yaliyoanza Disemba 11 na kilele chase kitafikia Disemba 17 mwaka huu.

Kalisti amesema wameanzisha mashindano ya watembea kwa miguu pamoja na waendesha baiskeli kwa lengo la kuhamasisha utalii katika hifadhi hiyo.

"Kesho ndio kilele cha shuhuli yetu hii ambayo tumeipa jina la Walkerthon and Adventure, ndani ya Msitu wa Magamba ambapo watu watatembea ndani ya msitu, watu wengi wa Lushoto hawajui kama wana rasilimali kubwa ndani ya wilaya yao".

"Ni msitu wa zaidi ya mita za mraba 9000 na kuna vituo vingi vya utalii, kuna mabwawa, vinyonga, maporomoko ya maji lakini pia kuna ndege aina mbalimbali hivyo niwaombe watu wajitokeze kwa wingi kutembelea msitu wetu" amesema.


Hata hivyo amebainisha kwamba katika kipindi cha miezi mitatu tayari zaidi ya Watalii 170 wa ndani na nje wametembelea katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wake Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi ya Msitu wa Asili Magamba (CSO) Christoganus Vyokuta amesema uhamasishaji huo ambao umewashirikisha Ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umelenga kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kmpeni yake ya The Royal Tour.

"Kuanzia Disema 16 mpaka kufikia leo tumeanza kuonesha vivutio vilivyoko ndani na wafanyabiashara ili kuhakikisha wananchi wanaifahamu vema wilaya yao lakini pia ikiwa ni juhudi za kuunga mkono utalii aliouanzisha Rais wetu" amesema.

Aidha amesema kuwa wako bega kwa bega na Ofisi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha kwamba kila kinachoanzishwa ngazi ya juu na huku tunatekeleza na kwamba kutakuwepo na mashindano mbalimbali katika matembezi hayo na mwamko wa washiriki ni mzuri.

"Mpaka sasa tuna washiriki zaidi ya 130 ambao wamethibitisha kushiriki matembezi ya km 5, 10 na 15 na pia kutakuwa na washiriki wa baiskeli, leo tunategemea watalii wa ndani na nje ya wilaya kwenda kulala ndani ya Hifadhi.

Msanii wa Bongo Fleva, Pamela Daffa (Pam D) ambaye ni mdau na mzawa wa wilaya ya Lushoto name amewataka wananchi kwenda kudhuhudia vivutio katika Hifadhi ya Msitu huo ili kuendeleza na kukuza utalii wa ndani pamoja na kuunga mkono filamu ya The Royal Tour.

"Wilaya yetu imebarikiwa kuwa na vitu vingi ambavyo vinasababisha waru wengi kuja kututembelea, tunayo Magamba Nature Reserve, mlima Kiguluhakwewa, tuna Irente View Point, lakini pia tuna Germany Caves pamoja na Maporomoko ya Maji".

"Vilevile tuna vyakula vya asili pamoja na uoto wa asili ambao uliweza kudumishwa zaidi ya miaka 100, yapo mambo mengi mazuri takuvutia na hii misitu tunayoiona ina miti zaidi ya 1000" amefafanua.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...