WAANDAAJI wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager 2024 wamewakumbusha washiriki kwamba wana siku chache kufurahia kipindi cha punguzo la awali ambapo watalipa chini ya kiingilio halisi kama wakijisajili kabla ya Desemba 14, 2023.

Taarifa iliyotolewa na waandaji inasema dirisa la awali limefunguliwa na washiriki wanaweza kutumia fursa hii kujisajili kwa wingi na kufurahia kipindi cha punguzo kwa kuepuka msongamano dakika za mwisho.

“Dirisha la awali la usajili lilianza Oktoba 16 na litaendelea hadi usiku wa manane wa Desemba 14 na baada ya hapo kiingilio kitapanda katika makundi yote na kwa mataifa yote kutoka Desemba 15 hadi Februari 5 2024 au hadi tiketi zitakapomalizika kutokana na kuwa na nafasi finyu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Waandaji walisema washiriki wanaweza kujisajili kupitia Tigopesa kwa kupiga *150*01#, kisha bonyeza 5 LKS, kisha bonyeza 5 (tiketi) na fuata maelekezo kujisajili au kwa njia ya tovuti rasmi www.kilimanjaromarathon.com. “Hii inatumika kwa makundi yote ya mashindano ya mbio, ikiwa ni pamoja na Kilimanjaro Premium Lager 42km (mbio za masafa marefu kamili), 21km (nusu ya mbio za masafa marefu ya Tigo Kili) na 5km (mbio za burudani),” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Waandaaji walisema zaidi kwamba usajili utasitishwa kabla ya siku ya tukio lenyewe Februari 25, 2024 wakati toleo la 22 litakapofanyika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kuhakikisha tukio linafuata Kanuni Rasmi za Riadha Duniani.

Hii, kwa mujibu wa waandaji, ni kuhakikisha wakimbiaji wanafurahia muda wao njiani bila ya kuwa na msongamano kupita kiasi kwa kuhakikisha kuna msaada wa maji na matibabu unaohitajika unapatikana njiani na wakati wa kumaliza na washiriki wote wanahudumiwa.

Kilimanjaro Premium Lager ni mdhamini mkuu wa mbio za masafa marefu na imeshika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa mbio za masafa marefu miaka 22 iliyopita.

Wadhamini wengine wa tukio la mwakani ni pamoja na wa nusu mbio za masafa marefu Tigo-21km, Gee Soseji mbio za Km 5, wadhamini wa meza za maji Simba Cement, Kilimanjaro Water na TPC Sugar. Wabia rasmi ni – KiliMedair, Garda World Security, CMC Automobiles, Sal Salinero Hotel na wasambazaji rasmi – Kibo Palace Hotel na Keys Hotel.

Mashindano ya mbio ya mwakani yatafanyika Jumapili ya Februari 25, 2024 Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na yatahusisha mbio za masafa marefu ya IAAF (42km), nusu ya mbio za masafa marefu (21km) na mbio za kujifurahisha (5km).

Tukio limeandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa na Executive Solutions limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...