Na Saidi Saidi, WMJJWM - Iringa

Wafanyabiashara ndogo ndogo mkoani Iringa wameishukuru Serikali kwa hatua ya kuwatengea maeneo rasmi ya kufanyia bisahara kwa utulivu.

Pongezi zimetolewa wakati wa ziara ya ufuatiliaji inayoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kupitia Kitengo cha Makundi Maalum Desemba 13, 2023 mkoani humo.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana, Afisa Biashara wa Manispaa ya Iringa Fadhil Mangoma amesema kuwa, kwa sasa hali ya wafanyabiashara ndogo ndogo mkoani humo ni salama na shughuli zinaendelea vizuri bila kero zozote.

"Serikali licha ya kutujengea masoko sita mkoani hapa ikiwepo Manispaa ya Iringa, imejenga mabanda 224 kwa ajili ya wamachinga kufanyia baishara zao na kuwafanya wamachinga wafanye biashara zao kwa utulivu tofauti na hapo zamani," amesema Mangoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Wilaya ya Iringa Mjini Kessy Michael, ameeleza mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili wamachinga kwenye masoko hayo, ikiwapo ukosefu wa wateja hivyo wao kama viongozi wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa wanawezesha vyombo vya usafiri kama bajaji daladala zinapita katika maeneo hayo na kuweka stendi ndogo ili kurahisiha usafiri.

Naye Afisa Maendelo ya Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Jeremiah Mwambange amewapongeza viongozi wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya usimamizi na uratibu wa shughuli hizo ili kuhakikisha biashara zinafanyika bila kuwepo na changamoto.

Mwambange amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, zitashirikiana na viongozi hao kuhakikisha wanatatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...