Na; Mwandishi Wetu - Bujumbura, BURUNDI


Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kuchangamkia fursa za Soko Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA). 
Rai hiyo imetolewa na Afisa Forodha Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Donald Tindamanyire wakati akiwasilisha mada kuhusu “Umuhimu wa Kuwandaa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Kuchangamkia Fusa za Soko Huru la Biashara kwa Wajasiriama” kwenye maadhimisho ya “SIKU YA TANZANIA” yaliyofanyika jijini Bujumbura tarehe 10 Desemba 2023 kwenye maonesho ya Nguvu Kazi/Jua Kali.
 Bw.  Tindamanyire amesema  kuwa wajasiriamali wana nafasi kubwa katika kutumia soko hilo la Afrika na kueleza kuwa kinachohitajika sasa ni wajasiriamali hao kujifunza taratibu mbalimbali zinazohitajika kwenye kulifikia soko hilo zikiwemo sheria, taratibu na kanuni za ufanyaji biashara za kuvuka mipaka ili kuepuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza pindi wanapohitaji kutumia soko hilo.

Vile vile, amewashauri wajasiriamali kuboresha na kuongeza thamani ya bidhaa zao pamoja na kutumia teknolojia ili kuzalisha kwa wingi na kuweza kuingia kwenye ushindani na nchi zingine za Afrika.

Pia Bw.  Tindamanyire alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake na vijana kutumia fursa ya soko hilo ambalo limeandaa Itifaki mahsusi kwa ajili ya kundi hayo.

Itifaki ya Soko Huru la Biashara Barani Afrika hadi sasa imeridhiwa na nchi 47 kati ya 54 za Afrika ikiwemo Tanzania na imeanza kutumika tangu mwezi Januari 2021.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...