Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro

WAKAZI wa Wilaya ya Same na maeneo jirani wakiwemo pia wafanyabiashara na wadau mbalimbali walio katika sekta ya utalii wametakiwa kujitokeza kushiriki tamasha la Same Utalii Festival lililopangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 18 hadi Desemba 20, 2023.

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema maandalizi yamekamilika lengo ni kuunga mkono jitihada zilizokwisha anzishwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kutangaza sekta ya Utalii kitaifa na Kimataifa.

"Zipo fursa za maonesho ya vyakula vya kiutamaduni,biashara zinazohusiana na Utalii,kuendeleza na kurithisha vizazi tamaduni za watu wa Kilimanjaro hasa Wapare , kuna utalii wa kuona wanyama pori hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwemo Faru weusi na Mbwa mwitu pia kupanda Mlima Shengena."

Amesema mgeni rasmi kwenye tamasha hilo la Same Utalii Festival anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasuli na Utalii Angela Kairuki huku akifafanua tamasha hilo litakuwa la kihistoria.

"Itakua fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa ndugu zetu Wapare ambao ninwenyeji, ndugu zangu mnaokuja ukanda huu wa mikoa ya Kaskazini kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka hii ni fursa kubwa na muhimu kwenu kushiriki tamasha la Same Utalii Festival, " amesema Kasilda Mgeni.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...