Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msofe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, akiwatunuku vyeti, tuzo na zawadi, Wanafunzi waliofanya vizuri kwa Mwaka wa masomo 2022/2023.Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2023 jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msofe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ametoa wito kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kusoma kwa bidii kwani ushindi na kutambuliwa kunatokana na kufanya vizuri kunajituma, kusoma kwa bidii na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wakufunzi katika masomo.

Ameyasema hayo leo Desemba 06, 2023 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti, tuzo na zawadi, Wanafunzi waliofanya vizuri kwa Mwaka wa masomo 2022/2023.

Amesema kuwa Utaratibu wa kuwatambua Wanafunzi wanaofanya vizuri ni mzuri kwani unachochea ukuaji na maendeleo ya kitaaluma katika taasisi.

Pia amewatia moyo wale ambao hawajapata tuzo, cheti na zawadi kwamba waruhusu fikra zao zitambae, kwani chuo kinamazingira mazuri na wanataaluma ambao wametengenezwa kwa namna hiyo.

"Natumaini kwamba kila mwanafunzi aliyesajiliwa katika taasisi hii anayonafasi ya kujifunza kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yake na kustahili kupata tuzo na zawadi kama wenzao waliopata kwa mwaka wa masomo 2022/ 2023.

"Tafadhali mjiwekee malengo na kuweka juhudi ili kufikia malengo hayo, mjitahidi kufanya mambo kwa namna tofauti na mtafute watu waliofanikiwa na kujifunza kutoka kwao." Amewaomba Prof. Msofe

Amesema watumieni mwanya huo kuwa nje ya boksi ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.

Pia amewapa moyo kwenye kufanya vitu ambavyo havifahamiki vifikie kufahamika kwani inapendeza na inafanya maisha kuwa marahisi.

Pia amewashukuru na kuwatambua wafadhili ambao wametoa zawadi kwaajili ya wanafunzi waliofanya vizuri wa DIT.

"Mchango huu si tuu unahamasisha wanafunzi kupenda fani, bali unaonesha kiu yenu ya kuona mafanikio makubwa na maendeleo katika fani mbalimbali zinazotolewa DIT." Amesema Prof. Msofe

Amesema tuzo ni njia mojawapo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao na kuleta ushindani miongoni mwao.

"Hii ndio sababu vyuo vikuu vingi na taasisi nyingi zimekuwa zikiandaa sherehe za utoaji tuzo kwa muda mrefu sasa, kufanya hivi kunawajengea wanafunzi bidii na kujiamini katika masomo yao na katika shughuli nyingine za ziada ikiwemo michezo na uongozi."

Pia amewahimiza taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kuendelea kuandaa tukio kama hilo mhimu na kuongeza wigo wa tuzo zinazotolewa kwa Wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi ya wenzao.

Prof. Msofe amesema Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia itaendelea kushirikiana na DIT ili kuboresha utoaji wa tuzo na kuhamasisha wanafunzi kuendelea kuwa wabunifu na kujifunza zaidi.

Kwa Upande wa Mwanafunzi aliyefanya vizuri wa shahada ya kwanza ya Telecom and Telecommunication, Jesca Alex amesema kuwa amepokea kwa furaha ushindi huo pia ameona ni kitu kizuri kwani wanatoa hamasa kwa wanafunzi wanajiunga na chuo hicho ili kufanya vizuri katika masomo yao.

"Nimeona inaleta dhamani na inaleta hamasa zaidi na inaonesha kudhaminiwa kwani tuzo zao nyingine zimetoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Universal Communications Service Access Fund (UCSAF)." Amesema Jesca


Mwanafunzi aliyefanya vizuri wa shahada ya kwanza ya Telecom and Telecommunication, Jesca Alex akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kutunuku cheti, kama mwanafunzi aliyefanya vizuri kwa Mwaka wa masomo 2022/2023.Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2023 jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msofe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti, tuzo na zawadi, Wanafunzi waliofanya vizuri kwa Mwaka wa masomo 2022/2023.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Profesa Preksedis Ndomba (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti, tuzo na zawadi, Wanafunzi waliofanya vizuri kwa Mwaka wa masomo 2022/2023.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...