Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mitaaa (TAMISEMI) amemtaka Mtendaji Mkuu wa TARURA, Victor Seff kuandaa mpango mkakati wa ujenzi wa barabara za vijijini na mijini nchi nzima unaolenga kukamilisha ujenzi wa barabara hadi kufika mwaka 2025 zikiwa zimejengwa kwa kiwango cha lami au teknolojia mbadala.

Mchengerwa ameongeza kuwa teknolojia mpya imefanyiwa majaribio hivi karibuni hivyo itatumika kama mbadala wa ujenzi wa barabara za lami ili kufikia lengo la zaidi ya asilimia 85 ya barabara za mijini na vijijini kuwa zenye kiwango sawa na cha lami.

Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa daraja la Bibi Titi, Mohoro-Rufiji, iliyofanyika leo Mkoani Pwani akisisitiza kuwa teknolojia hiyo ni ya uhakika ambapo barabara zitakazojengwa zitakuwa na uwezo wa kudumu kwa takribani miaka 20.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Barabara za Vijijini na Mijini, Mhandisi Venant Komba amesema teknolojia hiyo mpya imefanyiwa majaribio [pilot study] Dodoma na Mufindi ambapo kwa koa wa Dodoma imejengwa barabara ya Chamwino ya kilomita 6.7 ambapo ujenzi wake unaendelea na Mufindi ujenzi wa barabara ya Sawaya-Iyegeya ya kilomita 10 imekamilika.

Mhandisi Komba amesema teknolojia hiyo ni rafiki wa mazingira na inagharama nafuu zaidi ikilinganishwa na barabara yenye kiwango cha lami lakini pia ujenzi wake ni mwepesi zaidi kwani unatumia malighafi zilizopo eneo husika unapofanyika mradi.

 

Waziri  wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa akizungumza na wakazi  wa Muhoro mkoani Pwani Wilaya ya Rufiji.
 

Mkurugenzi wa Barabara za Vijijini na Mijini,Mhandisi Venant komba akieleza juu mradi huo utakavyo kuwa kwa wakazi wa Muhoro Rufiji Mkoani pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...