Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipita katika moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika kijiji cha Gendabi, Katesh mkoani Manyara. Mheshimiwa Majaliwa yupo mkono humo kujionea hali ya athari iliyosababishwa na mafuriko.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kukutana viongozi wa mkoa huo na wa Serikali na kupokea taarifa ya hali halisi ya tukio la maafa lililotokea jana na kusababisha vifo na majeruhi.

Waziri Mkuu alitoa pole kwa viongozi na wananchi wa Hanang kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumatatu, Desemba 4, 2023) kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, vyombo vua ulinzi na usalama na Watendaji wa taasisi za Serikali.

Waziri Mkuu amesema tukio la jana linafanana na tukio jingine lililowahi kutokea mwaka 1990 katika eneo la Ndanda ambako mlima uliporomoka na kusomba nyumba na barabara, hali ambayo ilisababisha vifo na majeruhi.

Amezishukuru Kamati za Maafa za Wilaya na Mkoa ambazo zilianza kuchukua hatua za uokoaji tangu jana, lakini pia mawaziri na watendaji wao ambao walikuja kutoa msaada kwa kuungana na viongozi wa mkoa wa Manyara.

Amesema matibabu yanaendelea kutolewa kwa majeruhi ambapo timu ya madaktari bingwa kutoka Dodoma, Singida na Arusha imeungana na kuanza kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa watatu waliovunjika mifupa.


Amesema majeneza yameagizwa kutoka Babati na Singida ili ndugu waliotambuliwa waweze kuhifadhiwa kwenye nyumba zao za milele.


Hivi sasa, Waziri Mkuu na baadhi ya mawaziri wamekwenda kukagua eneo la Mlima Hanang kwa kutumia helikopta. Eneo hilo ndiko maporomoko ya udongo yalianzia. Baadaye atashiriki kuaga miili ya marehemu na ndipo taarifa rasmi itatolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...