Na Ali Issa Maelezo 21/12/2023.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma amesema katika jitihada za kumlinda mtoto na ukatili wa kijinsia, Serikali imefanya Mapitio ya Sera na Sharia ya Mtoto ili ziende sambamba na wakati uliopo na mahitaji ya sasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipo kuwa akielezea Mafanikio yaliofikiwa kwa Wizara hiyo ikiwa ni kuelekea kilele cha miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar amesema mpango huo utafanikiwa kwa kuendelea kuzisimamia Sera ya Maendeleo na Sharia ya Mtoto ya Mwaka 2001 na Sharia ya mtoto nambari sita ya Mwaka 2011.

“Ili kuweka utekelezaji bora wa sharia ya kumlinda Mtoto zipo kanuni na sharia zimeandaliwa ambazo ni pamoja na kanuni ya matunzo na hifadhi ya mtoto,makazi na malezi”,alisema Waziri.

Aidha alisema kuanzishwa mazingira ya makazi kwa watoto kupewa huduma za kuwalea watoto na kuwatunza kwa kuhamishiwa jengo jipya la kisasa liliopo Mazizini zitaendelea kwani watoto hao awali walikuwa wanaishi farodhani.

Mbali na hayo alisema kuwa Serikali imefanikiwa kuwapatia Wazee Pensheni jamii , zaidi ya Wazee 29,000 waliotimia umri wa miaka 70 wanapatiwa shilingi elfu 50,000 kitu ambacho kwa nchi za Afrika bado hakija fikiwa.

Hata hivyo Waziri huyo alisema katika kusimamia usawa wa jinsia ,Wizara imeanda sera ya jinsia ya Zanzibar ya Mwaka 2016 pamoja na Serikali kukubaliana na Wadau wa Maendeleo katika kuandaa Sera ya maendeleo ya jamii itayowapatia jamii maendeleo katika Nchi.

Hata hivyo alisema Serikali itaendelea kuwatunza Wazee kwa kuwapatia Makazi bora na salama kwani kila Mtu ni Mzee Mtarajiwa hivyo kuwaekea mazingira mazuri na huduma za matibabu bure ni jambo lamsingi kwani kila mmoja wetu akiendelea kuwa hai basi uzee ajuwe unamnyemelea.

Waziri alitowa wito kwa jamii kuwaunganisha Wazee kwa Masheha waliofikia miaka 70 ili na wao wapate posho linalo tolewa na Serikali.

Hafla ni muendelezo wa vikao baina ya Mawaziri wa Wizara mbali mbali na Waandishi wa Habari katika kuelezea maendeleo, malengo na mafanikio ya Wizara zao, kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma akijibu maswali ya Waandishi katika Mkutano  kuelezea mafanikio na Changamoto ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Zanzibar.
 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma akitoa hotuba katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea mafanikio na Changamoto ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Zanzibar.
 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma akifafanua jambo wakati akitoa hotuba katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea mafanikio na Changamoto ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.21/12/2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...