Tani 150,000 za Korosho ghafi zimesafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutumika kikamilifu kwa Bandari hiyo kusafirisha korosho zote ghafi zinazolimwa Katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA) Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi amesema tangu kuanza kwa msimu wa korosho Bandari hiyo imehudumia Meli zaidi ya 18 za makasha, Meli tatu zikiwa zimeleta makasha matupu na Meli 15 zimesafirisha Korosho ghafi.

“ Mpaka sasa tumeshasafirisha tani laki moja na nusu na mpaka mwishoni mwa Januari tutakuwa tumeshasafirisha tani laki mbili. Tunakushukuru sana Serikali kwa maelekezo yake ambayo yameongeza ufanisi wa Bandari.” Amesema Nyathi.

Aidha amewashukuru Wadau wa Bandari na kampuni ambazo ziliamua kuwekeza katika Bandari hiyo ikiwamo Kampuni ya kuhudumia Makasha ya CMA na kampuni ya Meli ya Mediteranian Shipping kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha usafirishaji wa korosho ghafi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...