Na Mwandishi Wetu, Same
MBUNGE Wa jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro Anne kilango Malecela amechangia Sh. milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mtundu iliyopo Kata ya Mahole Same.
Akizungumza baada ya kuchangia fedha hizo, Kilango amesema shule zinazohitaji ujenzi zipo nyingi katika jimbo lake na shule nyingine tayari Rais Dk. Samia Suluhu Hassani ameshazijenga na tayari watoto wameingia darasani.
Akielezea fedha alizotoa amesema zitasaidia kuanza ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja katika shule ya Msingi Mtundu na Serikali Kuu imehaidi kusaidia ujenzi huo ili madarasa yakamilike kwa wakati.
Aidha amewapongeza wananchi wa Kata ya Mahole kwa juhudi binafsi katika nyanja mbalimbali za maendeleo hasa eneo la elimu.
"Hapa ninapozungumza tayari wananchi hawa kwa nguvu zao wamejenga Msingi wa madarasa mawili kwa hatua za maandalizi ya ujenzi wa awali bila kusubiri serikali, "amesema Kilango.
Mbali ya mchango huo zaidi Kilango amewatia moyo wananchi hao kuendelea na mshikamano huo kwa kuhakikisha wanasonga mbele katika kufanikisha shabaha iliyopo ya ujenzi wa ofisi na madarasa Matatu ya Shule ya Mtundu
Amewataka wananchi wa Kata ya Mahole kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi kubwa anayoifanya hasa Katika kuleta Maendeleo kwenye Taifa letu
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mahole Issa Rashid amempongeza Kilango kwa jitihada zake zote kupambana katika kushiriki katika ujenzi huo na kwamba hiyo inawapa moyo wananchi kuendelea kuchangia ujenzi huo.
Amesema Mbunge wao ametuonesha upendo wa dhati kwa watoto wetu na Sisi tutaendelea kushirikiana naye bega kwa bega hasa Katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...