Na Mwandishi Wetu

Kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoikumba Wilaya ya Hanang, Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) imetao saruji mifuko 1,000 ya saruji ikiwa ni kama msaada kwa jamii zilizoathirika.

Saruji hiyo itatumika kasaidia ujenzi wa nyumba zaidi ya 101 ambazo Serikali imepanga kuwajengea waathirika wa maafa hayo ya aina yake

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bi Queen Sendiga alisema "Maafa ya hivi karibuni yaliyotokea katika Wilaya ya Hanang yameziacha jamii zetu katika uhitaji mkubwa, msaada wa ukarimu wa kibinadamu kutoka kampuni ya EACOP umekuja kama mwanga wa matumaini katika nyakati hizi za changamoto.

Tunashukuru kwa mwitikio na msaada wao katika kusaidia juhudi zetu za kujenga upya na kurejesha maisha ya kawaida ya jamii kutokana na janga hili”

Maporomoko makubwa ya ardhi hususani miteremko mikali ya Mlima Hanang yameathiri maeneo ya miji ya Katesh na Gendabi. EACOP inatambua wajibu wa kushikamana na jamii zilizoathiriwa na janga hili, hasa kwa kuzingatia kuwa Wilaya ya Hanang ni mojawapo ya maeneo ambayo bomba letu linapita.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa EACOP Tawi la Tanzania, Bi. Catherine Mbatia alisema kuwa "Mchango wetu wa msaada wa kibinadamu ni ushuhuda tosha wa dhamira yetu katika kusaidia wenye uhitaji na unasisitiza dhamira yetu ya uwajibikaji wa kampuni katika jamii"

Maafa hayo yamegharimu maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa katika mashamba, na kupelekea maelfu ya watu kupoteza na kuhama makazi yao. Katika kukabiliana na maafa haya, EACOP imechangia mifuko 1,000 ya saruji ili kutoa msaada muhimu kwa wahanga wa mafuriko katika Wilaya ya Hanang.

Mmoja wa wanufaika wa msaada wa kibinadamu alisema kuwa "Napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa msaada wa EACOP. Msaada uliopokelewa utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazotukabili, na kutoa faraja na ahueni kwa familia zilizoathirika. Ushirikiano huu kati ya EACOP na jamii ni mfano bora unao onesha umoja katika nyakati za shida ”

EACOP inaamini katika nguvu na kuchukua hatua kwa pamoja, na hivyo imedhamiria kutumia rasilimali zake ili kuchangia ipasavyo katika kurejesha maisha ya kawaida na kujenga upya jitihada za wilaya.

Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya EACOP ya uwajibikaji wa shirika katika majukumu na msaada wa kijamii, kwa kutilia mkazo dhamira yetu katika ustawi wa maeneo tunapofanyia kazi. Kampuni inathamini umuhimu wa kuwa shirika la kiraia linalowajibika na linalothibitisha muunganiko wa shughuli zetu na jamii tunazozihudumia.EACOP itafanya kazi kwa karibu na serikali za mitaa na viongozi wa kijamii katika kutoa msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (kushoto) akipokea sehemu ya mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) Catherine Mbatia (kulia) ikiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yalifanyika Wilayani Katesh jana
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (Wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) Catherine Mbatia (kulia) ikiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yallifanyika Wilayani Katesh jana. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Hanang na EACOP.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) baada ya kupokea msaada wa mifuko 1,000 ya saruji iliyotolewa na bomba hili ikiwa ni msaada wa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yaliyofanyika Wilayani Katesh jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...