MWANDISHI WETU.

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)imewataka
Wadau, mashirika na taasisi mbalimbali kutumia masoko ya mitaji kama sehemu ya kukusanya mitaji kwa shughuli mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Afisa uhusiano na elimu kwa umma CMSA, Stella Anastazi, katika kilele cha maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara visiwani Zanzibar.

Stella amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ina dira ya kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha maendeleo ya uchumi wa bluu katika upande wa magharibi wa bahari ya hindi.

"Tukiangalia katika dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 imeiweka sekta ya uchumi wa bluu kuwa ndio sekta kuu ya kukuza uchumi Zanzibar,"amesema Stella.
Amesema masoko ya mitaji na dhamana ni moja kati ya mshirika mkuu kuhakikisha taasisi na mashirika mbalimbali yanapata mitaji kwa ajili ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali hapa Zanzibar na Tanzania bara.

"Sekta ambazo zimepewa kipaumbele kikubwa katika uchumi wa buluu ni Utalii, Uvuvi, nishati, usafiri wa baharini na usimamizi wa bahari hivyo wanaweza kupata mtaji wa kuwekeza katika shughuli zao kupitia njia ya kutoa hatifungani ya buluu ambayo inapatikana katika masoko ya mitaji na dhamana na kupitia hatifungani hii watapata mitaji ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali zitakazozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari,"amesema.

Aidha Stella amezitaka taasisi, wadau na mashirika mbalimbali kufanya mpango wa kutoa hatifungani za buluu na kutumia kikamilifu masoko ya mitaji ili waweze kujipatia mtaji ambao utawezesha ufanisi wa shughuli zao ili kuisaidia Serikali kufikia dira ya 2050 ya kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha maendeleo ya uchumi wa buluu.

Amesema maonesho ya Kimataifa ya Biashara hapa Zanzibar yamewezesha CMSA kupata wawekezaji wapya ambao wameingia katika bidhaa mbalimbali ikiwemo Hisa.

"Mwaka ndio kwanza umeanza naamini watanzania wataendelea kujitokeza zaidi katika masuala ya uwekezaji na ndio maana CMSA tumekuwa tukiwafikia katika maeneo mbalimbali na kuwapa elimu zaidi juu ya nini kinaendelea katika masoko ya mitaji,"

Kwa namna ambavyo wananchi wanazidi kutamani kujua umuhimu wa masoko ya mitaji imekuwa vyema kwao kuwapa elimu zaidi na zaidi kama ambavyo wanafanya hadi vyuoni.
Maonesho haya ya kimataifa ya biashara yameendana sambamba na maadhimisho ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo CMSA iliona ni vyema kujumuika na wananchi kuwapa elimu ya masoko ya mitaji.

Maonyesho hayo ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yamefikia tamati leo Visiwani hapa ambapo mwaka huu yamefanyika eneo la Dimani Fumba.



Afisa uhusiano na elimu kwa umma kutoka CMSA Stella Anastazi akitoa elimu ya uwekezaji kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo huko katika maonesho ya biashara Zanzibar ( Zanzibar International Trade Fair)
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...